Home LOCAL DESTURI NZURI NA ZENYE MADHARA KWA MAENDELEO YA JAMII SHINYANGA

DESTURI NZURI NA ZENYE MADHARA KWA MAENDELEO YA JAMII SHINYANGA

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.

 

Na: Kadama Malunde – Malunde 1 blog, SHINYANGA.

Wadau wa haki za wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga wameendesha majadiliano ya pamoja yenye lengo la kuibua mila na desturi nzuri zinazofaa kuendelezwa na zile zenye madhara zinazotakiwa kutokomezwa katika jamii.

 

Kikao kazi hicho cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga kimefanyika leo Alhamisi Desemba 23,2021 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na Wawakilishi kutoka Halmashauri za mkoa wa Shinyanga, viongozi wa dini, makundi maalum, wazee wa mila na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza shughuli zao katika eneo la mila na desturi.

 

Kikao hicho kimeongozwa na mada za Ushiriki wa wavulana na wanaume katika kukuza usawa wa kijinsia, wajibu wa jamii katika uimarishaji wa mila na desturi zinazolinda haki za wanawake na watoto na hatua dhidi ya aina zote za ukatili wa kijinsia ikiwemo ukatili wa kisaikolojia,kingono na kiuchumi katika jamii.

 

 

Akifungua Kikao hicho, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary amesema suala la kubadili mila na desturi siyo jambo la siku moja hivyo ni vyema kila mmoja katika jamii akashiriki katika kuleta mabadiliko ya mila na desturi ili kuhakikisha kunakuwa na usawa baina ya wanawake na wanaume.

 

“Tunataka kulenga kuleta usawa baina ya wanawake na watoto, tunataka kutokomeza mimba na ndoa za utotoni,ukeketaji,mtoto wa kike kubaguliwa kwa kutopewa elimu na ukatili wa kila aina”,amesema.

 

“Kila mmoja akemee mila potofu zinazokandamiza wanawake na watoto. Hata wale wanaopinga, waliong’ang’ania mila kandamizi wakiwemo wazee wa mila ambao hawajapata elimu ya masuala ya ukatili wa kijinsia ni lazima tuwashirikishwe ili tuwabadilishe wawe mabalozi wa kulinda wanawake na watoto”,amesema Omary.

 

 

Amesema baada ya kuanzisha majadiliano hayo kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga, mijadala zaidi itafanyika katika ngazi ya jamii.

 

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Juma Samwel amesema lengo la kuendesha majadiliano hayo ya pamoja ni kuibua mila na desturi nzuri zinazofaa kuendelezwa na zile zenye madhara zinazotakiwa kutokomezwa.

 

“Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto (Idara kuu ya maendeleo ya jamii) inaratibu utekelezaji wa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA). Katika mpango huu eneo namba 2 linahusu kutokomeza mila na desturi zinazokinzana na maendeleo na hivyo kukwamisha haki na ustawi kuleta madhara kwa jamii”,amesema Samwel.

 

“Ili kukabiliana na mila na desturi zenye kuleta madhara kwa jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto inakamilisha Mwongozo wa Kitaifa wa Majadiliano Ngazi ya Jamii ambao utatumika kuandaa majukwaa kwa ajili ya jamii kupata fursa ya kujadiliana ipasavyo juu ya kuwepo kwa mila na desturi ambazo ni nzuri ili ziendelezwe na zile ambazo zina madhara ziundiwe mikakati ya kuzitokomeza”,ameeleza.

 

Akichangia hoja wakati wa majadiliano hayo Hakimu kutoka Shinyanga, Doris Willson amesema Mahari kubwa ni chanzo cha ndoa za utotoni katika jamii.

 

“Mtoto akiolewa kwa ng’ombe wengi mfano 70 anafanyishwa kazi nyingi,mtoto akikua anakuja mahakamani kuomba, mahari kubwa inasababisha ndoa zinavunjika kwa sababu ya mateso wanayokutana nayo, matokeo yake talaka zinazidi kuongezeka”,amesema.

 

Naye Mchungaji Harold Mkaro kutoka Kanisa la KKKT Makedonia Shinyanga amesema ndoa nyingi za utotoni zimesababisha ndoa kuvunjika kutokana na maumivu waliyopata watoto hao yakiwemo ya kukosa elimu na kunyanyaswa.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Khamis Balilusa amesema ni vizuri sasa wana Shinyanga wakaangali mila zipi zinapaswa kuendelezwa na zipi kuachana nazo ili kuhakikisha kunakuwa na ustawi mzuri wa wanawake na watoto.

 

ZIFUATAZO NI PICHA MBALIMBALI.

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga kilichofanyika leo Alhamisi Desemba 23,2021 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. (Picha zote na: Kadama Malunde – Malunde 1 blog).
 

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
 
Mkurugenzi Msaidizi Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Juma Samwel akizungumza wakati wa kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
 

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga , Tedson Ngwale akizungumza kwenye kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
 

Mwalimu Silas Samaluku kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI akizungumza kwenye kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
 

Afisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto (Idara kuu ya maendeleo ya jamii), Avelino Chaulo akisoma maazimio ya kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
 

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Khamis Balilusa akichokoza mada kwenye kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
 

Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija akichangia hoja kwenye kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
 

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Tanzania na Mkoa wa Shinyanga Nancy Kasembo akichangia hoja kwenye kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
 

Hakimu – Shinyanga Doris Willson akichangia hoja kwenye kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
 

Mchungaji Harold Mkaro kutoka Kanisa la KKKT Makedonia Shinyanga akichangia hoja kwenye kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
 

Wadau wakiwa kwenye kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
 

Wadau wakiwa kwenye kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
 

Wadau wakiwa kwenye kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
 

Wadau wakiwa kwenye kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
 

Wadau wakiwa kwenye kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akipiga picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
 

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akipiga picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha majadiliano kuhusu mila na desturi nzuri na zenye madhara kwa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga.
Credit – Malunde 1 Blog
 

Previous articleUWT MKOA WA NJOMBE WAMPONGEZA RAIS SAMIA KULIONGOZA TAIFA VYEMA
Next articleMAJALIWA AHANI MSIBA NYUMBANI KWA KIKWETE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here