Na: Mwandishi wetu, DAR.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kikanda kutoka Wizara ya Mambo ya nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agness Kayola amekitaka Chuo cha Diplomasia hapa nchini kuongeza utafiti na ushauri elekezi ili kuweza kukabiliana na changamoto zinazozikabili Bara la Afrika ikiwemo ugaidi, mabadiliko ya tabia ya nchi, mapigano ya wahasi na uharifu wa bahari.
Balozi Kayola ameyasema hayo leo Disemba 1,2021 alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula kwenye Maafali ya Chuo hicho yaliyofanyika kwenye ulumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa Chu hicho kimekuwa kikifanya vizuri kwa kutoa wahitimu bora wenye uwezo wa kufanyakazi katika ngazi mbalimbali zikiwemo za Kimataifa na hivyo kukitaka chuo hicho kusimamia kwa ukaribu miradi ya chuo hicho iliyoko kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Aidha amewapongeza wanafunzi wote waliohitimu masomo yao katika ngazi tofauti nakwamba hiyo ni hatua muhimu ya kielimu na kuwahimiza kuwa elimu hiyo iwe chachu ya kujiendeleza zaidi kielimu na kutatua changamoto zinazo ikabili jamii.
“Nyie ni tegemeo la taifa yetu hivyo mnawajibu wa kulinda na kuenzi taifa letu,” amesema.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Chuo Cha Diplomasia Balozi Dk.Abdulrahman Kaniki amesema kuwa katika kuimarisha maofisa wa Serikali na Sekta Binafsi ili kuendana na mabadiliko yanayotokea Duniani, chuo hicho kimeendesha kozi fupi ambazo ni Diplomasia ya uchumi, Ofisa uhusiano na Itifaki, Itifaki na uhusiano wa Serikali, usuluhishi wa migogoro na amani na zinginezo.
Amesema kuwa mpaka sasa Chuo hicho tayari kimezalisha zaidi ya mabalozi 20, waliopangiwa katika mataifa mbalimbali na watumishi zaidi ya 102 wanaofanya kazi katika Wizara ya mambo nje ushirikiano wa Afrika Mashariki na kikanda waliopangiwa ofisi mbalimbali na kuipongeza Wizara hiyo kwa kuwapokea wanafunzi 100 kwaajili ya kupata mafunzo kwa vitendo.
“Changamoto tuliyonayo nipamoja na ukosefu wa sehemu za kutosha kuwapeleka wanafunzi kujifunza kwa vitendo,” amesema.
Nakuongeza kuwa “Pia alisema chuo hicho kinaendelea kushirikiana chuo cha huria cha Dar es Salaam(Open University), Zanzibar institute of (EPA) na kinafanya utaratibu wa kuhimarisha ushirikiano na vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi, vinavyoendana na maudhui yao, ilikubadilishana uzoefu,” ameongeza.