Na:Stella Kessy
TIMU ya soka la ufukweni leo imetinga katika hatua ya fainali dhidi ya Msumbiji katika mashindano ya COSAFA yanayofanyika Durban, Afrika Kusini.
Tanzania imetinga hatua hiyo ya fainali baada ya kuichapa Angola bao 5-2 ,huku kila timu ikitamani kuibuka na ushindi dhidi ya mpinzani wake, huku mchezaji bora katika mechi hiyo ameibuka toka Tanzania ambaye Stephano Waile.
Katika mchezo mwingine ulikuwa katika ya Comoro iliibuka na ushindi wa bao 8-6 dhidi ya Seychelles, Msumbiji iliibuka kidedea dhidi ya wenyeji Afrika Kusini kwa ushindi wa bao 5-3.