Na: Stella Kessy
TIMU ya Taifa ya soka la Ufukweni jana imeibuka mshindi wa pili baada ya kuchapwa na Msumbiji mabao 3-1 fainali ya mashindano ya COSAFA yanayofanyika Durban, Afrika Kusini.
Ushindi huo ni mwendelezo wa ubabe wa Msumbiji kwa Tanzania, kwani mechi ya Kundi B walishinda kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 4-4.
Mechi nyingine Tanzania iliyo chini ya kocha Boniphace Pawasa ilishinda 3-1 dhidi ya Comoro Kundi A kabla ya kuifunga Angola 5-2 kwenye Nusu Fainali
Akinzungumza na mwandishi wa stori hii Kocha mkuu wa kikosi hicho Boniface pawasa amesema kuwa mchezo ulikuwa na ushindani na wapinzani wao walifanikiwa kupata ushindi wa matokea hayo.
“Tulipambana na mwisho mshindi amepatika sina budi kukubali matokeo lengo letu lilikuwa kuwa bingwa wa michuano hiyo lakini tumeshika nafasi ya pili tunamshukuru mungu kwa hatua ambayo tumepata” amesema
Ameongeza kuwa kikosi kinajipanga kuja na sasa wapo safari watawasili kesho majira ya saa tano asubuhi hivyo anawaomba watanzania na wadau kuiombea katika safari yao ili kuweza kuwasili salama.