Home SPORTS TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI SOKA LA UFUKWENI

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI SOKA LA UFUKWENI


Na: Stella Kessy

TIMU  ya Taifa ya soka la Ufukweni jana imeibuka mshindi wa pili baada ya kuchapwa na Msumbiji mabao 3-1 fainali ya mashindano ya COSAFA yanayofanyika Durban, Afrika Kusini.

Ushindi huo ni mwendelezo wa ubabe wa Msumbiji kwa Tanzania, kwani mechi ya Kundi B walishinda kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 4-4.

Mechi nyingine Tanzania iliyo chini ya kocha Boniphace Pawasa ilishinda 3-1 dhidi ya Comoro Kundi A kabla ya kuifunga Angola 5-2 kwenye Nusu Fainali

Akinzungumza na mwandishi wa stori hii Kocha mkuu  wa kikosi hicho Boniface pawasa amesema kuwa mchezo  ulikuwa na ushindani na wapinzani wao walifanikiwa kupata ushindi wa matokea hayo.

“Tulipambana na mwisho mshindi amepatika sina budi kukubali matokeo lengo letu lilikuwa kuwa bingwa wa michuano hiyo lakini tumeshika nafasi ya pili tunamshukuru mungu kwa hatua ambayo tumepata” amesema

Ameongeza kuwa kikosi kinajipanga kuja na sasa wapo safari watawasili kesho majira ya saa tano asubuhi hivyo anawaomba watanzania na wadau kuiombea katika safari yao ili kuweza kuwasili salama.

Previous articleBOCCO AWAPIKU MANURA, ZIMBWE JR, TUZO ZA IDFA
Next articleDR NDUMBARO TUTAPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA MTINDO MPYA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA UHURU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here