Home BUSINESS DR NDUMBARO TUTAPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA MTINDO MPYA MAADHIMISHO YA MIAKA 60...

DR NDUMBARO TUTAPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA MTINDO MPYA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA UHURU

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha kuhusiana na upandaji wa mlima Kilimanjaro katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru.
 
Faustine Chombo mtaalamu kuongeza wapanda mlima kutoka kampuni ya ZARA TOUR akielezea maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru
 
NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

Wizara  ya maliasili na utalii imepanga kusherhekea maadhimisho  miaka 60 ya Uhuru kwa kupanda mlima Kilimanjaro kwa mtindo mpya na wa  tofauti na uliozoeleka  ambapo zaidi ya watu 300 wanatarajia kushiriki katika zoezi hilo.

Hayo yameelezwa na waaziri wa maliasili na utalii Dkt Damas Ndumbaro katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika mkoani Arusha ambapo alisema kuwa zoezi hilo litaanza December 5 mwaka huu na kati ya watu 300, 120 wameshathibisha kushiriki.

Dkt Ndumbaro alisema kuwa wizara yake  kwa kushirikiana na kampuni ya ZARA tours ambao ndio waandaji wa zoezi hilo wamepunguza gharama za kupanda mlima huo hadi kufikia laki nane kwa siku saba hadi nane ili kila mtanzania mwenye nia ya kupanda aweze kupanda.

Alifafanua kuwa mlima kilimnjaro una historia kubwa ya nchi na ni sehemu pekee ambapo unaweza kuona barafu equtor lakini pia mlima huo ni alama ya uzalendo kwa nchi hivyo watanzania waupigiganie na kukulinda kwa maslahi endelevu ya kizazi cha sasa na baade.

“December 9, 2021 tunaadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika na kama tunavyojua  miaka 60 ni umri wa mtu mzima kwahiyo nchi nayo imepiga hatua kubwa na sisi kama wizara ya maliasili na utalii tumeamua kusherhekea kwa namna ya kipekee, kwa njia tofauti na  kwa maeneo tofauti ya nchi hii na mojawapo ni kupanda mlima Kilimanjaro, tunajua watu wamepanda miaka mingi lakini hii itakuwa ya kipekee kutokana na mtindo tukatumia kupanda,” Alieleza Dkt Ndumbaro.

Alisema kuwa zoezi la kujisajili kwaajili ya kupanda mlima katika maadhimisho hayo yanafanywa na kampuni ya kitalii ya ZARA ambao wanaoshirikiana na serikali kuratibu zoezi hilo na mpaka sasa watu zaidi ya 120 wameshajisajili na kasi ni kubwa hivyo na wengine wajitokeze ili kuweza kufikia kiwango kilichowekwa.

Kwa upande wake Faustine Chombo mtaalamu kuongeza wapanda mlima kutoka kampuni ya ZARA TOUR alisema kuwa hadi sasa maandalizi yameshakamilika na wamejipanga kutoa huduma iliyo bora kwa wapandaji wote siku hiyo hivyo watanzania wajitokeze kwa wingi kwani wamejiandaa vya kutosha.

“Maandali ni mazuri na tuna vifaa vipya  vinavyoendana na wakati, vyakula vya kutosha na waongozaji wa kutosha ambao wamebobea katika kazi hiyo na niseme tu kuwa wakati umefika kwa watanzania kujua umuhimu wa hifadhi  zetu na uzuri ni kwamba gharama ni nafuu badala ya kulipa milioni mbili Hadi tatu kwasasa ni laki 8 na hamsi tuu,”Alisema.

Hata hivyo zoezi hilo lenye kauli mbie kukutane kileleni ni maalum kwaajili ya watanzania wote lakini pia ni sehemu ya kukumbuka juhudi zilizifanywa na waasisi wa nchi katika kuleta Uhuru. 


Previous articleTANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI SOKA LA UFUKWENI
Next articleMASHIRIKA YASIYO YAKISERIKALI KENYA YAKABIDHI HATI YA KULIOMBA BUNGE LA EALA KUINGILIA KATI SUALA LA USAWA WA KIJINSI KATIKA UONGOZI NCHINI KENYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here