Home SPORTS TAIFA STARS YACHAPWA 3-0 NYUMBANI

TAIFA STARS YACHAPWA 3-0 NYUMBANI

 

 

Mwandishi wetu 

TIMU ya  Tanzania (Taifa Stars) leo imepoteza kwa kichapo cha  mabao 3-0 dhidi ya Congo katika mbio za kufuzu  Kombe la Dunia katika mchezo uliochezwa  Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Leopards yamefungwa na kiungo wa Lille ya Ufaransa, Gael Romeo Kakuta Mambenga dakika ya sita, beki wa Cape Town City ya Afrika Kusini, Nathan Idumba Fasika na mshambuliaji wa Sharjah ya Dubai, Ben Malango Ngita dakika ya 85.

Kwa matokeo hayo, Leopards inapanda kileleni mwa Kundi J ikiizidi pointi moja Taifa Stars kuelekea mechi za mwisho Jumapili.

Mechi nyingine ya Kundi hilo itachezwa Saa 1:00 usiku baina ya wenyeji, Benin wenye pointi saba pia na Madagascar yenye pointi tatu Uwanja wa l’AmitiĆ© Jijini Cotonou.

Kundi limezidi kuwa gumu kwa sababu sasa timu yoyote unaweza za kusonga mbele, kwani Madagascar wakishinda mechi mbili za mwisho watamaliza na pointi tisa na Taifa Stars inaweza kufuzu ikishinda mechi ya mwisho na endapo Benin na DRC zitatoa sare Jumapili Kinshasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here