Home BUSINESS STAMICO, BENKI YA NMB WAINGIA MAKUBALIANO KUWAINUA WACHIMBAJI WADOGO

STAMICO, BENKI YA NMB WAINGIA MAKUBALIANO KUWAINUA WACHIMBAJI WADOGO

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse (kulia), na Afisa Mkuu wa Mikopo kutoka Benki ya NMB Daniel Mboto (kushoto) wakibadilishana hati ya makubaliano ya kuwakopesha wachimbaji wadogo, mara baada ya kutia saini makubaliano hayo kwenye Ofisi za STAMICO Jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse (kulia), na Afisa Mkuu wa Mikopo kutoka Benki ya NMB Daniel Mboto (kushoto) wakisaini hati za makubaliano hayo Jijini Dar es Salaam. 


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse (wa pili kulia), na Afisa Mkuu wa Mikopo kutoka Benki ya NMB Daniel Mboto (wa pili kushoto) wakionesha hati za makubalino mara baada ya kutia saini makubaliano hayo. (wa kwanza kulia) ni, Mwanasheria wa STAMICO , na (wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Idara ya Biashara, Benki ya NMB Alex Mpeno, wakipiga makofi kupongeza kufanikiwa kwa zoezi hilo. 

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse (kulia) akizungumza kabla ya zoezi la kutia saini hati za makubalino hayo. (kushoto) ni, Afisa Mkuu wa Mikopo kutoka Benki ya NMB Daniel Mboto.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse, akisisitiza jambo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa hafla hiyo. 
Afisa Mkuu wa Mikopo kutoka Benki ya NMB Daniel Mboto, akizungumzia mikakati yao ya kuwainua kiuchumi wachimbaji wadogo, wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini makubaliano na Shiririka la Madini la Taifa (STAMICO), leo Novemba 22,2021 Jijini Dar es Salaam.

Wadau mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse kwenye Hafla hiyo.
Mkuu wa Idara ya Biashara, Benki ya NMB Alex Mpeno, ( wa kwanza kulia), akiwa na Meneja Mwandamizi Idara ya Biashara wa Benki hiyo Christopher Mganzi (katikati) wakisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu wa Mikopo kutoka Benki ya NMB Daniel Mboto. (hayumo pichani) wakati wa Hafla hiyo.
Mwakilishi wa Wachimbaji wadogo Salma kundi kutoka TAWOMA akizungumza kwenye hafla hiyo kuishukuru STAMICO, kwa na NMB kuwawezesha kufikia malengo yao.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa STAMICO Bibiana Ndumbaro akizungumza alipokuwa akiwakaribisha waandishi wa habari kwenye hafla hiyo. 
(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO).
 
TAZAMA VIDEO.

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

SHIRIKA la Madini la Taifa Stamico leo limeingia makubalino na Benki ya NMB kwa  kutiliana saini ya mashirikiano ya kuwainua wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwapatia mikopo ili waweze kuendeleza shughuli zao.

Akizungumza katika hafla fupi ya kutiliana saini makubaliano hayo yaliyofanyika kwenye Ofisi za STAMICO Jijini Dar se Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa  STAMICO Dkt Venance Mwasse amesema kuwa Shirikia hilo lina jukumu kubwa la kuwasimamia na kuwasaidia wachimbaji wadogo hapa nchini nakwamba mpaka sasa wameshatoa  leseni za uchimbaji wazawa zaidi ya elfu 30 hapa nchini.

Amesema kuwa ili katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wanaimarika kiuchumi wamekuwa na mikakati mbalimbali ya kuwasaidia ikiwemo kuwaunganisha na Taasisi za Kifedha ikiwemo Benki ya NMB kutoa mikopo kwa wachimbaji hao ili kuendeleza shughuli zao za uchimbaji.

“Makubaliano haya  yanakwenda kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwa wachimbaji na hivyo yatanufaisha pande zote mbili  kwa maana ya benki na wachimbaji ambao ni wateja.” Amesema

Ameongeza kuwa kuwa makubaliano hayo yanakwenda kutengeneza ukuaji wa kodi, nakwamba kutakuwa na mzunguko mkubwa wa fedha na kuwataka wachimbaji hao kufuata sheria ili waweze kufikia malengo yao.

Ameongeza kuwa STAMICO wamenunua mashine tano kwa ajili ya uchorongaji ambazo ndio mwarobaini kwani zitakuwa msaada mkubwa kwenye shughuli za uchorongaji na kuwawezesha kupata uhakika wa uwepo wa madini katika eneo husika .

Kwaupande wake  Afisa Mkuu wa Mikopo kutoka Benki ya NMB Daniel Mboto ameishukuru STAMICO kushirikiana nao katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wananufaika nakwamba leo la makubaliano hayo ni kukuza na kuleta mabaadiliko chanya katika sekta ya madini.

“Kupitia ushirikiano huu Benk ya NMB itashirikiana na STAMICO kuhakikisha wateja walioko kwenye sekta ya Madini wanapata muongozo na msaada sahihi wa matumizi ya fedha zao katika shughuli zao”Amesema Mboto.

Ameongeza kuwa STAMICO wanatakiwa kuwa na taarifa sahihi za mchimbaji huyo ili hata atakapopatiwa mkopo aweze kuaminika na kuhudumiwa.

“Nawashukuru sana stamico kwa kufikia makubaliana haya ambayo yanakwenda kuwa na tija katika  nchi na kwa wachimbaji hawa wadogo.”amesema.

Ameongeza kuwa watatoa elimu ya fedha kwa wadau katika sekta ya madini ili kuwasaidia katika kuhakikisha wanakuwa na matumizi sahihi ya fedha.

“Ni fursa ya kipekee sana kwa wachimbaji wadogo na wadau wa sekta ya madini kwani kwa kila hatua ya shughuli zao ,Benki ya Nmb na STAMICO tuko nao kuhakikisha wanafanikiwa.” amesema

Alifafanua kiwa mteja anapata muongozo wa namna ya kuwekeza na wapi pakuwekeza kutoka Stamico ,baadae benki ya Nmb inampa mkopo rafiki kabisa wakati mteja anaendelea na shughuli zake.

“Nitoe rai kwa wadau wa sekta ya madini kuchangamkia fursa hii na watembelee matawi ya Nmb kwa ajili ya maelekezo ya mikopo ambayo kwa sasa itakuwa na baraka na miongozo kutoka Stamico na kuwafanya wapige hatua mbele zaidi katika biashara na shughuli zao.” amesema

Kwa upande wake mwakilishi wa wachimbaji wadogo Salma kundi kutoka TAWOMA aliwashukuru Stamico na kwamba  kwao ni siku ya kihistoria na kwaniaba ya wachimbaji wadogo wote amesema wao watajitahidi kwakufuata utaratibu wote ili waweze kunufaika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here