Na: Stella Kessy
KOCHA mkuu wa klabu ya Simba Pablo Franco amesema kuwa kwa ushindi waliopata itasaidia wachezaji wake kujiamini katika mchezo wa kombe la shirikisho Afrika.
Kauli hiyo ametoa leo kuwa kikosi chake kimecheza vizuri katika kipindi cha kwanza na kupata matokea ya mabao matatu japo kuwa walitengeneza nafasi nyingi lengo lilikuwa kupata ushindi mnono.
Amesema kuwa simba ni timu kubwa inastahili kupata zaidi ya walichopata leo hivyo wataendelea kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza ili kiwa imara.
“Ni ushindi muhimu tumepata japo nilizungumza na wachezaji kuhusu hili tunajua tunaongeza morali kuelekea mchezo wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows”amesema.
“Tumecheza vizuri hasa kipindi cha kwanza lakini tunastahili kupata zaidi ,simba ni timu kubwa na tunahitaji kurudi Kwenye ubora wetu hivyo tunapaswa kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza “amesema Pablo.