Na: HERI SHAABAN (ILALA)
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala, Mohamed Msophe amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Wazazi za Jumuiya hiyo.
Saruji hiyo alikabidhi Kata ya Buyuni leo kwa Mwenyekiti wa Wazazi Kata Ally Juma Wambanguru
“Kampeni ya kujenga ofisi za Jumuiya ya Wazazi ni Kampeni yangu endelevu kila Kata iwe na ofisi yake nikiwa Mwenyekiti wa Wazazi nitahakikisha nasimamia Jumuiya hii vizuri pamoja na chama” alisema Msophe
Msophe alisema mpango huo ni endelevu Wilaya nzima kuwa na ofisi ya Jumuiya kwa ajili ya kukisaidia chama na Jumuiya zake ziweze kufanya Kazi zake kwa ufanisi.
Msophe alisema Wilaya llala ina Kata 36 mpango wa ujenzi kila Kata iwe na Ofisi ya Jumuiya ya Wazazi kwa ajili ya kulinda siri za chama na Jumuiya.
Mwenyekiti Msophe aliwataka viongozi wa Jumuiya ya Wazazi kila Kata kuwa wabunifu kwa kubuni miradi mbalimbali ndani ya Jumuiya hiyo.
Msophe alisema Mikakati yake kuijenga upya Jumuiya ikiwemo kuongeza wanachama wapya ndani ya Jumuiya sambamba na kukijenga Chama cha Mapinduzi
Alisema Jumuiya ya Wazazi ni Jumuiya mama inalelewa na chama cha Mapinduzi dhumuni kuimalisha Jumuiya kifikie malengo yake sambamba na Chama cha mapinduzi .
Mwenyekiti Msophe alisema haiwezekani jumuiya ya wazazi waendelee kuishi kwa kupanga ofisi lazima wawe na mikakati ya kuwa na ofisi zao .
Aliwaomba viongozi wa wazazi kata kuweka mikakati ya kujiimarisha kiuchumi ikiwemo kuimalisha miradi ya Jumuiya hiyo.
Aliwataka makatibu Kata na Matawi kuongeza Wanachama sambamba na kuwa wabunifu kwa ajili ya kubuni miradi ya jumuiya kwa ajili ya kujiwezesha kiuchumi.
Aidha aliwaomba viongozi wote wa kata na matawi kuanzisha vikundi vya wanawake na walemavu wanaotokana na Jumuiya hiyo ili vipate mikopo ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambayo aina riba kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Mwisho.