NA: MANDISHI WETU
MBUNIFU wa mavazi nchini Irfan Riziwanali, amefunguka sababu ya Tanzania kushindwa kufanya vizuri katika mashindano ya mitindo na urembo duniani.
Irfan ni moja ya wabunifu ambao wameishi nje ya nchi kwa muda mrefu kwa kipindi hichi cha miaka miwili amejikita katika ubunifu wa mavazi hapa nchini ana miliki duka la mavazi Masaki jijini Dar es Salaaam.
Akizungumza na ukurasa huu amesema nchi za wenzetu wanachukua muda mrefu, kuwa andaa wawakikishi wao na kuwapatia mafunzo mbalimbali ndiyoo sababu ya wao kufanya vizuri.
“Hatufanyi vizuri katika mashindano ya urembo duniani kwa sababu wawakilishi wetu hawapati muda mrefu wa kujiandaa na kupatiwa mafunzo nchi za wenzetu wana anza mapema kuwa andaa wawakukishi wao tokea wakiwa shuleni,” anasema Irfan.
Anaeleza kuwa ili kufanya vizuri katika mashindano hayo kwanza jamii iwe na muamko na tasnia hii, pia serekali ianze kutoa mafunzo mashuleni kwa wale watoto ambao wanaonyesha kupenda kuwa wana mitindo.
“Tuna somo la Stadi za kazi ndani yake kuna vitu vingi ambavyo watoto wanafundishwa itapendeza kama mitindo ikiwa moja ya mada ambazo zinafundishwa kwa undani zaidi hii ita saidia kukuza tasnia na kufanya vizuri katika mashindano ya dunia.”