Na: Damian Kunambi
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga ametembelea na kusaidia shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea katika kata mbalimbali wilayani humo uliotokana na fedha za uviko 19.
Mbunge huyo ndani ya siku mbili tayari ametembelea shule za sekondari zilizopo katika kata sita ambazo ni sekondari Kayao, Madilu, Lugarawa, Ikovo, Mundindi pamoja na shule ya sekondari mavanga na bado anaendelea na ziara yake katika kata nyingine zaidi.
Mbuge huyo amesema katika kata ambazo amedika amekutana na changamoto upatikanaji hafifu wa saruji ambapo kutokana na zoezi hilo la ujenzi kuwa la nchi nzima limepelekea saruji kupungua na kutopatikana kwa wakati.
Aidha ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kulipatia jimbo lake kiasi cha sh. bilioni 1,210,000,000 ambazo zimekuwa ni msaada na kuwapunguzia wananchi michango ya mara kwa mara.
Amesema fedha hizo zimelenga maeneo mbalimbali ambapo vyumba 47 vya madarasa sekondari sh. 940,000,000 bweni wanafunzi wenye uhitaji maalum sh. 80,000,000, vyumba vya wagonjwa ICU shs. 100,000,000 na nyumba ya mtumishi sh. 90,000,000
“Changamoto hizi za madarasa na vituo vya afya zipo maeneo mengi katika jimbo langu hivyo ujio wa fedha hizi zimesaidia kutatua changamoto hizi kwa wananchi wangu”, amesema Kamonga.
Aidha kwa upande wa baadhi ya madiwani wa kata hizo wameishukuru serikali sambamba na kueleza juhudi walizonazo ili kukamilisha kwa wakati ujenzi huo.
Credit: Fullshangwe Blog.