Home SPORTS MAJALIWA: WATANZANIA WANATAMANI TIMU ZAO ZIFANYE VIZURI

MAJALIWA: WATANZANIA WANATAMANI TIMU ZAO ZIFANYE VIZURI


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa GSM, Gharib Mohamed (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Hasa Customs Clearance Company Limited, Salim Abdallah ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Oktoba 1, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa  Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa (wa nne kushoto), Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadau wa  mpira wa miguu nchini   kwenye ukumbi wa  Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 1, 2021. Wa tatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Caspar  Mmuya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa  Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa , Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadau wa  mpira wa miguu nchini   kwenye ukumbi wa  Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 1, 2021. Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Caspar Mmuya pia alihudhuria kakao hicho. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa  Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa (wa nne kulia), Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadau wa  mpira wa miguu nchini   kwenye ukumbi wa  Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 1, 2021. Wa tatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Caspar Mmuya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu,

)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa GSM, Gharib Mohamed (kushoto)na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Hasa Customs Clearance Company Limited, Salim Abdallah baada ya mazungumzo mafupi, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 1, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  

DODOMA.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Watanzania wanatamani kuona timu zao za Taifa za michezo mbalimbali zinafanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa.
 
Amesema kuwa uwezekano wa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) kufanya vizuri katika michuano ya kufuzu kombe la Dunia itakayofanyika nchini Qatar 2022 ni mkubwa kutokana na matokeo mazuri ambayo imeyapata katika michezo ya minne ya awali.
 
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Novemba Mosi, 2021) wakati wa kikao na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa , uongozi wa TFF pamoja na wadau wa mpira wa miguu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.
 
“Tukifanikiwa kushinda mechi hizo mbili zilizobaki kati ya timu ya Taifa na Congo pamoja na mechi ya timu ya Taifa na Madagascar ambayo itachezwa ugenini, itatupa matumaini ya kushiriki katika michuano ya kombe la dunia, hivyo Serikali inaamini ushirikiano kati ya wadau na Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni muhimu katika kufanikisha lengo hilo.”
 
Akiongea na wadau hao, Mheshimiwa Majaliwa amesema michuano ya kombe la dunia ni fursa kwa wachezaji wetu kwani itawasaidia kutambulika katika mataifa mbalimbali duniani hivyo kupata nafasi ya kuhitajika na vilabu vikubwa duniani.
 
“Tukishinda mechi hizi mbili pamoja na kuvuka hatua ya mtoano itakayotuwezesha kushiriki kombe la dunia tutakuwa tumewasaidia wachezaji wetu kupanua soko lao kimataifa kwa kuwa wataonekana na hata tutakapoita timu ya Taifa tutakuwa tunaita wachezaji wengi wa kimataifa tofauti na sasa ambao ni watatu tu nao ni Mbwana Samatta, Simon Msuva na Novatus Dismas”.
 
Waziri Mkuu amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema anatamani kuona timu ya Taifa soka ya wanaume (Taifa Stars) inafanya vizuri kama ilivyo kwa timu ya Taifa ya soka wanawake ambayo hivi karibuni ilichukuwa ubingwa kwenye mashindano ya kombe la COSAFA 2021 yaliyofanyika nchini Afrika Kusini.

 

Previous articleMATOLA AZUNGUMZIA UKOSEFU WA UMAKINI KWA WASHAMBULIAJI WAKE
Next articleSERIKALI YAPOKEA DOZI 500,000 ZA SINOPHARM.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here