Home BUSINESS BENKI YA ABSA YASHIRIKI MAONESHO YA WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA

BENKI YA ABSA YASHIRIKI MAONESHO YA WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA

 
Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Jamal Kassim Ally (wa pili kulia), akiwapungia mkono wafanyakazi wa Benki ya Absa, wakati akipita mbele ya banda hilo alipokwenda kufungua rasmi maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam, jana. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Mawasiliano Wizara ya Fedha, Benny Mwaipaja, Kamishna Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Charles Mwamaja na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangassa.

Mkuu wa Kitengo cha Bima wa Benki ya Absa, Sandeep Chavda (kushoto) akiwa na Mfanyabashara, Anic Kashasha wakati akitembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya wiki ya huduma ya fedha kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa Kitengo cha Wateja Maalum, Agnes Mushi.

Meneja Uhusiano wa wa Benki ya Absa, Victor Nchimbi (kulia) akitoa maelezo ya huduma za kibenki kwa mmoja wa wafanyabiashara waliotembelea katika banda la benki hiyo, Charles Mishetto wakati wa maonesho ya wiki ya huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Wengine ni maofisa wa benki hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Bima wa Benki ya Absa, Sandeep Chavda (kulia) akitoa maelezo kwa mfanyabiashara Thomas Masamaki kuhusu huduma za bima zinazotolewa na Absa wakati was a benki hiyo katika maonesho ya wiki ya huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Wengine ni maofisa wa benki hiyo.
Meneja wa Kitengo cha Wateja Maalum, Agnes Mushi (kushoto) akizungumza na mfanyabiashara Kawembe Hashimu wakati akitembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya wiki ya huduma za kifedha uanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Wengine ni maofisa wa benki hiyo.
Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Kaiser (kulia), akizungumza na baadhi ya maofisa wa benki hiyo wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam, jana. Kutoka kushoto ni, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Aron Luhanga, Meneja Mahusiano Wateja Maalumu, Veronica Magoyane, Meneja Kitengo cha Wateja Maalumu, Agnes Paul Mushi na Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Melvin Saprapasen.
Meneja Kitengo cha Mauzo wa Benki ya Absa, Fabian (katikati), akitoa maelezo kuhusu faida za akaunti ya Absa Junor Eagle kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Msimbazi walipotembelea banda la benki hiyo wakati wa maonyesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkuu wa Mauzo, John Maganga na kushoto ni Bahati Mwakaje wa kitengo hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here