Home SPORTS YANGA YAAHIDI POINTI TATU MCHEZO WA KESHO DHIDI YA GEITA

YANGA YAAHIDI POINTI TATU MCHEZO WA KESHO DHIDI YA GEITA

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

KIKOSI cha Yanga  kesho kinatarajia kushuka dimbani kuchuana na Geita Gold katika mchezo wa ligi kuu unaotarajiwa kuchezwa katika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa moja usiku.

Kikosi cha Yanga kinashuka dimbani kikiwa tayari kina jumla ya pointi tatu baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar 1-0 uliochezwa katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

kikosi cha Geita kitaingia uwanjani kikiwa na tahadhari kubwa baada ya kufungwa katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Namungo.

Katika mchezo huo ambao utakuwa wa ushindani  timu ya Geita  itatakiwa kulinda lango lao na kutafuta point tatu huku Yanga nao wakiwa na malengo ya kupata matokeo ili kuongeza pointi kwenye msimamo wa ligi.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Ofisa habari wa kikosi cha Yanga Hassan Bumbuli anasema kuwa kikosi kipo vizuri na kila mechi kwao ni fainali.

“Kwasasa hakuna mechi ndogo kwasasa na huu ni mwanzo mzuri kwa kushinda mechi ya kwanza dhidi ya Kagera Sugar na sasa tunakutana na Geita ambayo nina amini ni kubwa ndio maana inashiriki ligi kuu” anasema.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa mwalimu mkuu Kocha Narsedeen Nabi wachezaji wote wapo vizuri na wamejiandaa vya kutosha katika kupata matokeo  mazuri hapo kesho. Licha ya kuwakosa wachezaji Mukoko Tonombe ambaye anatumikia adhabu aliyopewa na bodi ya ligi ya kukosa michezo mitatu katika fainali za FA pia mchezaji Bakari Mwamnyeto ambaye anauguza majeraha

Aidha ameongeza kuwa klabu ya Yanga imelenga kuchukua ubingwa wa ligi kuu msimu huu pamoja na FA na kuendelea kutetea kombe la mapinduzi.

Katika mchezo huo tiketi zitauzwa  VIP A 15000 VIP B 1000 huku mzinguko ikiwa ni 5000

Previous articleTUPO TAYARI KUIKABILI YANGA KESHO: MANYASI
Next articleGST YAGUNDUA UWEPO WA MADINI YA DHAHABU LUMBANGA WILAYANI MALINYI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here