Home SPORTS TWIGA STARS YACHEZEA KICHAPO

TWIGA STARS YACHEZEA KICHAPO


Na;Stella kessy

TIMU ya Taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars leo imechezea kichapo 2-1 dhidi ya Namibia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa kufuzu AFCON ya mwakani Morocco.

Huku katika upande wa Namibia mabao yote yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Zenatha Goeieman Coleman dakika ya 22 na 61.

Huku wa upande wa Twiga Stars bao limefungwa na kiungo wa JKT Queens, Stumai Abdallah Athumani dakika ya 41.

Timu hizo zitarudiana Oktoba 23 Uwanja wa Dobsonville Jijini Johannesburg, Afrika Kusini na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Malawi na Zambia na atakayeshinda hapo amekata tiketi ya Morocco mwakani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here