Home SPORTS TANZANITE YAICHAPA ERITREA

TANZANITE YAICHAPA ERITREA

 

Na: Stella Kessy, Dar es Salaam.

TIMU ya Taifa ya wanawake (U-20), Tanzanite Queens imeibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Eritrea katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamanzi.

Mabao ya timu hiyo yamefungwa na nahodha Irene Elias Kisisa pamoja na Protasia Mbunda, kwenye mchezo wa marudiano wa kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia nchini Costa Rica 2022.

Katika ushindi huo Tanzanite imefuzu kwenye raundi ya pili kwa jumla ya mabao 5-0, baada ya awali kushinda kwa mabao 3-0, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Asmara, nchini Elitrea.

Baada ya raundi ya pili itafuatiwa na raundi ya tatu ambayo washindi wake wa jumla ndio watakaofuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Costa Rica mwakani.

Previous articleIDARA YA ELIMU HALMASHAURI YA JIJI YAPOKE MADAWATI
Next articleTWIGA STARS YABEBA UBINGWA WA COSAFA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here