Home SPORTS SIMBA KUTUPA KARATA NYINGINE KWA DODOMA JIJI LEO

SIMBA KUTUPA KARATA NYINGINE KWA DODOMA JIJI LEO


Na: Stella kessy.

KIKOSI  cha simba leo kinaingia uwanjani katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma jiji utakaopigwa katika dimba la Jamhuli.

Akizungumza na kwa niaba ya wachezaji wenzake  mlinzi wa kulia Shomari Kapombe  amesema kuwa  watajitahidi kupata matokeo katika mchezo wa leo ili kurudisha ari ya wachezaji na mashabiki.

Hata hivyo kikosi simba huu ni mchezo wa pili tangu ligi kuanza, baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Biashara United.

Amesema kuwa leo wanahitaji kupata matokeo ili kuridisha imani kwa mashabiki na kuleta morali kwa wachezaji. 

Hata hivyo Kapombe hatokuwepo katika kikosi cha kesho baada ya kupata majereha ya mchezo  dhidi ya Biashara.

simba leo inakutana dodoma jiji ambao waliwafunga Ruvu Shooting bao 2-0  katika mchezo uliochezwa dimba la Jamhuli jijini humo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here