Home SPORTS POULSEN: LIKOSI KIPO IMARA KUIKABILI BENIN

POULSEN: LIKOSI KIPO IMARA KUIKABILI BENIN

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Kim Poulsen amesema kuwa wachezaji wapo imara katika mchezo wa leo dhidi ya Benin

Kauli hiyo aliitoa kwa vyombo vya habari kwenye mkutano maalum na kusema kuwa wachezaji wa Benin wapo vizuri ila amejipanga kuchukua point tatu kwenye mchezo huo.

“Tumefanya mazoezi kwa siku mbili hivyo sasa ni nimeona wachezaji wapo vizuri katika mchezo kikubwa ninachoomba watanzania wajitokeza kwa wingi ili kuongeza hamasa kwa wachezaji” alisema.

Aliongeza kuwa wachezaji wapo katika hali nzuri nakwamba watarajie kuona soka bora zaidi kwenye mchezo huo.

Kwa upande  nahodha wa kikosi cha Stars John Bocco alisema kuwa wachezaji wamejipanga vyema katika kufanya vyema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here