Mwandishi wetu MOSHI.
POLISI Tanzania yaibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Katika mtanange huo mabao ya Polisi leo yamefungwa na Kassim Shaaban dakika ya 23 na Adam Adam dakika ya 40, wakati la Azam FC limefungwa na Iddi Suleiman ‘Nado’.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Coastal Union imetoa sare ya pili mfululizo nyumbani, 0-0 na KMC Uwanja wa Mkwawani, Tanga