Home BUSINESS MEYA KUMBILAMOTO AIPONGEZA BENKI YA BIASHARA TCB

MEYA KUMBILAMOTO AIPONGEZA BENKI YA BIASHARA TCB

NA: HERI SHAABAN.
MEYA waHalmashauri ya Jiji la Dar Salaam   Omary Kumbilamoto ameipongeza Benki ya Biashara Tanzania (TCB ) kwa kutoa huduma bora kwa Watanzania.

Meya  Kumbilamoto alitoa pongezi  hizo wakati akiwa  tawi la TCB Mbagala Chalambe Wilayani Temeke Dar es Salaam  jana katika madhimisho ya wiki    ya Wateja Benki ya Biashara Tanzania TCB.

“Naipongeza Benki ya Biashara Tanzania TCB (zamani ilikuwa ikijulikana benki ya Posta kwa kutoa huduma bora kwa jamii” alisema Kumbilamoto.

Meya Kumbilamoto aliwashauri TCB kujikita zaidi kwa Jamii  kusaidia Serikali  sekta ya Elimu na afya katika juhudi za kuisaidia Serikali ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha aliwataka TCB kuweka kipaumbele kwa wananchi wa Mbagala katika kutoa huduma bora na kuisaidia wananchi.

 

Kwa upande wake Meneja wa Tawi la Benki ya TCB Mbagala Edward Molela alisema tawi hilo limeanza kutoa huduma January mwaka huu zamani lilijulikana kama benki ya Posta Tanzania .

Meneja Edward alisema Benki hiyo ipo chini ya Serikali inatoa huduma kwa watu wa kipato cha chini na kipato cha kati.

Msimamizi wa Benki hiyo ya TCB Tanzania Godfrey Nyamuhama alisema kwa sasa mchakato wa Benki hiyo kuwa na kadi ya VISA benki yao ipo inamilikiwa na serikali kwa asilimia 98.

Godfrey alisema benki hiyo kwasasaa imewekeza zaidi  fursa kwa Wanawake katika  mikopo  inawanyanyua wanawake sekta ya uchumi na uzalishaji watanzania watumie benki ya TCB .
Mwisho.

Previous articleDKT.GWAJIMA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA USWIZI NCHINI TANZANIA
Next articleMAJALIWA: BARABARA YA NANGURUKURU-LIWALE KUJENGWA KWA LAMI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here