Home LOCAL MBUNGE BONAH AWATAKA WANANCHI KUACHA MAENEO YA HIFADHI YA BARABARA

MBUNGE BONAH AWATAKA WANANCHI KUACHA MAENEO YA HIFADHI YA BARABARA

Na: Kheri Shaaban.

MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli, amewataka wakazi wa Mtaa Msingwa Bonyokwa Wilayani Ilala kuacha maeneo ya Hifadhi ya Barabara  za ili zifanyiwe upanuzi.

Mbunge Bonah aliyasema hayo Dar es Salaam jana Mtaa Msingwa katika ziara ya Maendeleo kuangalia miundombinu ya barabara kwa ajili ya upanuzi ambapo alikutana na kero ya wananchi kujenga maeneo ya hifadhi ya barabara.

Bonah aliwashauri wananchi waliozidi kuacha maeneo hayo wazi  ili wataalam wakipita wasikose kuletewa Maendeleo ikiwemo kujengewa Barabara zao sambamba na kuchonga.“Maendeleo yoyote yanaletwa na wananchi wenyewe ,Wananchi wangu wa Msingwa tusizibe Barabara watalaam wa kija tukakosa kujengewa kwa kisingizio cha kuziba barabara zao za mitaa ambapo hata maeneo mengine greda kupita ni shida” alisema Bonah

Katika ziara hiyo ya jimboni kutatua kero alitembelea mtaa Msingwa na wataalam wa barabara wa Halmashauri ya Jiji na TARURA ambapo alisema miundombinu hiyo kwa sasa itaboreshwa na TARURA ikiwemo kuzichonga  wakati wakisubiri mradi wa awamu ya tatu wa kuboresha miundombinu.

Aliwataka wakazi wa  eneo la kwa makofia na Mjumbe Lukas wanatakiwa  kufuata sheria kwa kuacha maeneo wazi wasisibe njia miradi ikifika wasije toa sababu ya kushindwa kupitisha  Barabara.

Diwani wa Bonyokwa Wilaya Ilala Tumike malilo ,alimpongeza Mbunge Bonah kwa ziara hiyo ya utatuzi wa kero ambapo alifanya naye ziara maeneo yote  yenye changamoto ya miundombinu yao na maeneo yatakayowekwa kalabati .

Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Msingwa Hassani Ngimbi alisema ataanza kutoa Elimu kwa wananchi wake waheshimu Barabara ikiwemo kufanya vikao vyenye ajenda moja ya Maendeleo yao na kukubaliana kila mtu kuacha njia .

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here