Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na viongozi, wafanyakazi wa Posta na wananchi mbalimbali waliojitokeza katika siku ya Posta Duniani katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Dodoma. Oktoba 9,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akimkabidhi zawadi na cheti mshindi wa uandishi wa barua kutoka kundi maalum ambaye ni mlemavu wa macho Faraja Robert wakati wa maadhimisho ya siku ya Posta Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Dodoma . Oktoba 9, 2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akikata utepe kuashiria kukabidhi vitendea kazi yakiwemo magari na pikipiki kwa Shirika la Posta nchini nje ya ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Dodoma. Oktoba 9,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiendesha gari mojawapo katika ya magari aliokabidhi kwa Shirika la Posta mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya siku ya Posta Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya posta duniani yaliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Amewataka kuongeza jitihada katika kutangaza huduma za Posta ili jamii ipate kuelewa wa taswira mpya ya shirika hilo na kutumia huduma zinazopatikana. Amesema awali wananchi walichoshwa na huduma hafifu zilizokuwa zikitolewa na shirika hilo ambazo zilipelekea kupotea pamoja na kucheleweshwa kwa mizigo na fedha. Amesema ni muhimu shirika hilo kwa sasa kujikita katika misingi ya kibiashara na kuachana na tamaduni hodhi zilizopitwa na wakati.
Aidha ameiagiza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuendelea kusimamia kwa karibu Sekta ya Posta nchini ili iongeze mchango unaotakiwa katika pato la Taifa. Pia amewataka watoa huduma za posta binafsi kuhakikisha wanakua na leseni ya utoaji wa huduma hizo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameagiza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kujizatiti zaidi kwenye utafiti wa ukuaji wa teknolojia ili kurahisisha utendaji kazi za Serikali kwa ujumla huku akitoa rai kwa watanzania wote, taasisi na idara za serikali kutumia huduma za posta zilizoboreshwa kwa manufaa ya taifa.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Rahma Kassim Ali amesema huduma ya posta imekua msaada mkubwa Zanzibar kutokana na kuongezeka kwa biashara ya mtandao huku Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji amesema Shirika la Posta lina umuhimu mkubwa kwani hutumika katika kuwezesha biashara kimataifa na kutangaza utalii kupitia Stempu zenye alama mbalimbali za vivutio vilivyopo nchini.
Makamu wa Rais katika siku ya Posta Duniani amekabidhi vitendea kazi kwa Shirika la Posta nchini ambavyo ni magari 5 makubwa yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6 magari madogo 13, bilioni 1.1 , na pikipiki 20 zenye thamani ya shilingi milioni 60.6 ili kuongeza uwezo wa shirika katika kuwahudumia wananchi.