Home SPORTS KMC FC, NAMUNGO VITANI LEO MCHEZO WA LIGI KUU LINDI

KMC FC, NAMUNGO VITANI LEO MCHEZO WA LIGI KUU LINDI

 

Mwandishi wetu.

Kikosi  cha KMC FC  leo kinashuka katika uwanja wa Ilulu hapa mkoani Lindi kwenye mchezo wa mzunguko wa Nne Ligi kuu ya NBC Tanzania bara dhidi ya Namungo utakaochezwa saa 14:00 mchana.

KMC FC ambao ni wageni katika mchezo huo, walifika Lindi Oktoba 20 ambapo jana  na leo mchana  itafanya maandalizi yake ya mwisho kabla ya mchezo huo wa kesho na kwamba wachezaji , benchi la ufundi wamejiandaa kuhakikisha kwamba kama Timu inapata matokeo mazuri katika mchezo huo.

Akizungumza kwenye mahojiano na mwandishi wa blog hii  Afisa Habari na Mawasiliano wa KMC FC Christina Mwagala amesema Maandalizi ya mchezo huo yamefanyika kwa ustadi mkubwa ambapo kila mchezaji anamorali ya kuiwezesha Timu kushinda licha ya kwamba mchezo huo  utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na Timu zote mbili kutoka kupoteza mchezo wa mzunguko wa tatu.

Amesema kuwa licha ya kupoteza michezo michezo mitatu ambayo hadi sasa Timu ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu John Simkoko imeshacheza haijapata matokeo mazuri na kwamba mkakati uliopo ni kujipanga vizuri katika mchezo wa kesho ilikufanikisha adhma ya Timu kupata alama tatu kwani maandalizi yamefanyika vizuri.

“Tunajua tumetoka kupoteza mechi ngumu dhidi ya Yanga, na tunakwenda pia kwenye mchezo mgumu dhidi ya Namungo, lakini hii haitupi hofu na badala yake imetupa changamoto ya kuzidi kupambana hivyo kesho tunaenda kupambania alama tatu muhimu tukiwa ugenini hapa Lindi.

Lakini kikubwa tunamshukuru Mungu kwamba wachezaji wote wako salama hakuna mwenye majeraha na kwamba wote wapo tayari kuipambania Timu kwenye mchezo huo ambao kimsingi bado upo ndani ya uwezo wetu kwa maana ya kushinda licha ya ushindani tutakaokutana nao.

Kikubwa tunawashukuru mashabiki zetu kwakuendelea kutusapoti licha ya kuwa hatujakuwa na wakati mzuri tangu kuanza kwa Ligi kuu msimu huu, lakini niwahakikishie tu kwamba ushindi unakuja na tutapanda kwenye nafasi zetu ambazo mmezoea kuiona Timu yetu hivyo hakuna kukata tamaa.

Previous articleTAARIFA KWA UMMA, KUPUNGUA KWA UZALISHAJI MAJI MTAMBO WA RUVU CHINI
Next articleHABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO J.MOSI OCTOBA23-2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here