Home LOCAL TAARIFA KWA UMMA, KUPUNGUA KWA UZALISHAJI MAJI MTAMBO WA RUVU CHINI

TAARIFA KWA UMMA, KUPUNGUA KWA UZALISHAJI MAJI MTAMBO WA RUVU CHINI


23.10.2021

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inawataarifu wananchi na wakazi wa Bagamoyo Mkoani Pwani hadi Kigamboni Jijini Dar es salaam kuwa, kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji .

Sababu: Upungufu wa maji katika chanzo cha Mto Ruvu.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Maji kupitia Bonde la Wami Ruvu, kina cha maji cha mto Ruvu kimepungua kufuatia kiangazi cha muda mrefu.

Kufuatia upungufu wa maji mtoni, uzalishaji wa Maji umepungua kutoka lita milioni 520 kwa siku hadi kufikia lita milioni 460. Upungufu huo unatokana na kupungua kwa uzalishaji katika mtambo wa Ruvu Chini ambao husambaza maji kwa asilimia 70 ya eneo la huduma la DAWASA. Mtambo wa Ruvu Chini kwa kawaida huzalisha lita milioni 270 kwa siku na hivi sasa unazalisha kiasi cha lita milioni 210 kwa siku.

DAWASA kwa kushirikiana na Ofisi za Bonde la Wami Ruvu wanaendelea na zoezi la kusitisha matumizi ya maji kwa watumiaji wengine katika mto huo ikiwa ni pamoja kusitisha vibali vya umwagiliaji ili kuruhusu maji kufika mitamboni.

Ili kuhakikisha kuwa maji yanapatikana kwa usawa katika eneo linalohudumia na mtambo wa Ruvu Chini, DAWASA imehamisha sehemu ya maji ya Ruvu Juu ili yatumike kwa maeneo yaliyokuwa yanahudumiwa na Mtambo wa Ruvu Chini. Mabadiliko haya yanapelekea kupungua kwa msukumo wa maji kwa baadhi ya maeneo.

Maeneo yatakayo athirika: Maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Maji Ruvu chini, kuanzia Bagamoyo hadi Kigamboni.
DAWASA inawaomba wananchi kutumia maji kwa uangalifu katika kipindi hiki.

Tupigie kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 au ujumbe mfupi 0735202121 (WhatsApp)

Imetolewa na

Kitengo cha Mawasiliano na Jamii- DAWASA
Previous articleRAIS SAMIA ATUNUKIWA TUZO YA TEHAMA, AKABIDHIWA WAZIRI MKUU MAJALIWA KWA NIABA YAKE, JIJINI ARUSHA LEO
Next articleKMC FC, NAMUNGO VITANI LEO MCHEZO WA LIGI KUU LINDI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here