Uongozi wa Azam Fc umesema kuwa licha ya kufanya vibaya katika michezo miwili ya ligi kuu tangu sio kwamba kikosi kipo vibaya.
Kauli hiyo imetolewa na kocha msaidizi wa Azam, Vivier Bahati amesema kuwa kikosi bado kipo imara watakikisha wanapata pointi tatu dhidi ya Namungo hapo kesho.
“Naweza sema kuwa tumeanza vibaya lakini sio kwamba kikosi kibaya ninajivunia kuwa wachezaji wangu wapo vizuri kuhakikisha katika dimba la nyumbani ” amesema.
Kuelekea mchezo huo, Nahodha Msaidizi wa Azam FC, Bruce Kangwa, amesema kuwa kikosi kimejipanga kufanya vyema katika dimba la nyumbani.
“Unajua msimu huu tumeanza vibaya sio kwamba ndio tutaishi hivi bali tutazidi kusonga mbele na kupata matokeo mazuri katika mechi zijazo lakini pia tumepanga kufanya vyema kwa msimu huu ambao una ushindani sana” amesema
Amesema kuwa wameshaambiana wao kama wachezaji kuhakikisha wanapambana ili kufanya vema kwenye michezo ijayo.
“Sisi kama wachezaji tumejipanga vizuri wote tunajituma mazoezini, wote wanaonyesha wanataka kucheza mechi, unajua mechi ya kwanza ya ligi tumefanya vibaya na ya pili lakini mchezo huu wa tatu utakuwa ndio mwanzo wa matokeo ” amesema.
Kangwa aliwaomba mashabiki wa Azam FC wajitokeza kwa wingi kuwasapoti kwenye mechi zao na wao kama wachezaji watawapa matokeo wanayohitaji