Home SPORTS KATIBU MKUU NISHATI ASEMA MICHEZO ITUMIE KUBORESHA AFYA NA UFANISI KAZINI

KATIBU MKUU NISHATI ASEMA MICHEZO ITUMIE KUBORESHA AFYA NA UFANISI KAZINI

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja( wa tano kushoto) akikabidhi mpira kwa Mwenyekiti wa Michezo wa Wizara ya Nishati, Germanus Haule( wa nne kushoto), mara baada ya kutoa nasaha kwa wanamichezo hao, Octoba 18,2021 jijini Dodoma, wa tano kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara  hiyo, Ziana Mlawa.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Nishati Ziana Mlawa (katikati) akizungumza na wanamichezo wa wizara hiyo (hawapo pichani) walipokuwa wakipatiwa nasaha kabla ya kwenda kushiriki Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), mkoani Morogoro Octoba 18, 2021.

Mwenyekiti wa Michezo wa Wizara ya Nishati, Germanus Haule(aliyesimama)akiwaeleza jambo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Nishati Ziana Mlawa (mwenye kilemba) kabla ya kupewa nasaha za kwenda kushiriki Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI),mkoani Morogoro Octoba 18,2021.

Na: Zuena Msuya, DODOMA.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja ameiasa Timu ya Wanamichezo wa Wizara ya Nishati inayoshiriki Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), kutumia Michezo hiyo kama sehemu ya kuboresha Afya na ufanisi sehemu za kazi.

 

Mhandisi Masanja amesema hayo mkoani Dodoma wakati akitoa nasaha kwa wachezaji hao wanaokwenda kushiriki SHIMIWI mkoani Morogoro kuanzia Octoba 20 hadi Novemba 2, 2021.

 

Aidha amewataka wanamichezo hao kuheshimu Michezo hiyo na kuzingatia dhana nzima ya kuanzishwa kwake.

 

Vilevile aliwasihi wanamichezo hao kucheza kwa nidhamu pamoja na kuwa na mbinu za ziada ili kupata ushindi wa kishindo.

 

Sambasamba na hilo amewaeleza kuwa wanapokuwa kambini wanapaswa kuishi kwa nidhamu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa wizara hiyo Ziana Mlawa aliwaeleza wanamichezo hao kuwa wanapokuwa kambini ni sawa na wanapokuwa maeneo yao ya kazi hivyo wafuate na kuzingatia taratibu zote za kiutumishi.

 

Mlawa alisema kuwa wanamichezo hao wakawe mfano bora kiutendaji kwa kushiriki mazoezi ya aina yote na yale yote wanayopaswa kufanya wanapokuwa katika michezo hiyo.

 

Vilevile aliwasihi kuendeleza umoja, ushirikiano kwa wanamichezo wote watakaokuwa pamoja kama wanavyoshirikiana na watumishi wengine katika wizara ya Nishati.

  

Takribani wanachezo 30 kutoka Vitengo na Idara za wizara hiyo watashiriki michezo ya Mpira wa Pete, Miguu, kuvuta kamba, kuendesha Baiskeli, mbio za Magunia nk.

 

Michezo ya SHIMIWI inatajiwa kufunguliwa Octoba 20, 2021 na kufikia kilele chake Novemba 2, 2021 mkoani Morogoro.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here