Home LOCAL DIWANI MUSHI AWAUNGANISHA BODABODA KATIKA MIKOPO

DIWANI MUSHI AWAUNGANISHA BODABODA KATIKA MIKOPO


Na Heri Shaaban, Dar es Salaam.

DIWANI wa kata ya Kipunguni Steven, Mushi   ametoa elimu ya mikopo kwa madereva wa bodaboda na viongozi wao kwa ili wachangamkia fursa mikopo ya halmashauri.

Diwani Mushi alitoa elimu hiyo Dar es salam jana Dar es Salaam  na viongozi wa bodaboda kata ya kipunguni dhumuni la mafunzo hayo wachangamkie fursa ya mikopo ya serikali ambayo inatolewa ngazi ya halmashauri.

Mwitikio katika mafunzo haya ni makubwa mitaa yote minne wameshiriki mafunzo hayo yalioandaliwa na ofisi ya Diwani wa kata” alisema Mushi.

Mushi alisema dhumuni la kikao hicho ni mikakati yake ya kuwasajili katika vikundi ili watambulike wakope mikopo ya halmashauri ya vijana Wanawake na watu wenye ulemavu.

Aidha alisema katika mikakati hiyo ya kuwawezesha boda boda wameanza na vikundi 100 chini ya ufadhili Mbunge wa jimbo la ukonga.

Mushi aliwataka vijana wa bodaboda kuunda vikundi vya watu kumi na kuandaa ya umoja wao katiba ili wawe na sifa ya kuchukua mikopo ya serikali ambayo aina riba iliyotolewa na serïkali kupitia halmshauri kwa ajili ya kuwakwamua wananchi wakuze mitaji yao.

Alisema atawasimamia vijana wa kipunguni kuakikisha wanapata fursa hiyo waweze kupata mitaji na kujiajili wenyewe  wakuze mandeleo ya uchumi wa viwanda katika wilaya ya ilala katika kuunga mkono juhudi za Rais kupeleka fursa kwa wananchi .

Adha Diwani Mushi amewapatia ofisi bodaboda wa Kipunguni kwa ajili ya kufanyia majukumu yao mbali mbali katika utendaji wa kazi zao.

Aliwandalia mikataba Maalum ya bodaboda ambayo itakuwa wanatumia ndani ya kata hiyo kwa matajili wao ambayo ina maslahi kwao bila kuwa bana na matajili ili kulinda maslahi yao.

Aliwataka bobadaboda wote wa Kipunguni kujisajili serikali za mtaa ili watambulïke kwa usalama wa raia na mali zao.

Aliwataka madereva wa pikipiki wa kata ya Kipunguni kufanya kazi kwa weledi wasijiushishe na vitendo viovu kwani kazi yao ni ajira katika kusaidia jamii

Mwisho

Previous articleMAGAZETI YA LEO J.TANO OCTOBA 13-2021
Next articleSIMBA KUIFUTA GALAXY IJUMAA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here