Home ENTERTAINMENTS AGGY BABY AACHIA KIBAO KINGINE CHA ‘WATAJUAJE’

AGGY BABY AACHIA KIBAO KINGINE CHA ‘WATAJUAJE’

MALKIA  kwenye muziki wa Bongo fleva Agness Suleiman maarufu kama Aggy Baby leo 21 Oktoba  ameachia rasmi wimbo wake mpya unaoenda kwa jina la ‘WATAJUAJE’  wenye uhalisia wa uswahili (uswazi).
 
Kwa mujibu wa Aggy Baby amesema tayari wimbo huo unapatikana karibu kwenye ‘platform’ zote za muziki za mitandaoni ikiwemo Boomplay, Youtube,  iTunes,  Audiomack na zingine nyingi.
 
“Fans wangu na wadau wote wanaweza kuusikiliza wimbo wangu mpya kupitia mitandao karibu yote.
 
Ikiwemo Google play, TIDAL, Amazon na sehem zingine ikiwemo kwenye mitandao yangu ya kijamii kwa jina la @aggybaby_”  Alisema.
 
Wimbo huo wa ‘Watajuaje’ pia unaweza kuupata kupitia link hii: 
https://youtu.be/gxenVsl-AdU na kufuatilia kupitia kurasa zake ‘page’ za instagram Aggybaby_
Aggy Baby pia bado yupo kwenye chati za muziki akitamba na wimbo wake wa ‘WANIPA’.
 
Aggy Baby mbali ya kuimba pia ni rapa (Rapper),  msanii wa filamu (Actor), mtunzi na Mwandishi wa nyimbo na Mwanaharakati wa Vijana katika mambo ya kusaidia jamii.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here