Home SPORTS YANGA YAPOTEZA NYUMBANI

YANGA YAPOTEZA NYUMBANI

Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

KIKOSI cha Yanga leo wamepoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya River United bao 1-0 katika Ligi ya Mabingwa Afrika uliopingwa katika uwanja mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani.

Dakika 45 zilikamilika kwa timu zote kutoshana nguvu jambo ambalo liliwafanya waende kenye vyumba vya kubadilisha nguo ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 0-0 Rivers United .

Kipindi cha pili ngoma ilipinduka baada ya Rivers United kuongeza kasi ya mashambulizi na kupata kona ya kwanza dakika ya 50 iliyoleta bao lililopachikwa na nyota wao Moses Omdumuke .

Jitihada za Yanga kupitia kwa mshambuliaji wao Heritier Makambo ambaye alimpisha Ditram Nchimbi hazikuweza kuleta matunda na kuwafanya wapoteze furaha katika mchezo wa kwanza.

Yanga ina kazi ya kwenda kusaka ushindi nchini Nigeria kwenye mchezo wa marudio wa Ligi ya Mabingwa unaotarajiwa kuchezwa Septemba 18.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here