Home SPORTS YANGA YAAHIDI USHINDI DHIDI YA RIVERS UTD

YANGA YAAHIDI USHINDI DHIDI YA RIVERS UTD

Na: wandishi wetu,  Dar es Salaam.

UONGOZI wa Yanga umesema kikosi kipo vizuri na wachezaji wamejipanga  kwa ajili ya  mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United utakaopigwa leo majira ya saa 11 Katika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Leo Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa awali dhidi ya Rivers United kutoka Nigeria ambao wa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kauli hiyo aliitoa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa mashabiki wasiwe na presha juu ya wachezaji wao watatu kukosa vibali vya kazi, (ITC).

“Ukizungumzia Yanga hauzungumzii mchezaji mmoja ama wawili ni orodha ya wachezaji wa kazi zaidi ya mmoja na tumesajili wachezaji 30 hii ina maana kwamba akikosekana mmoja mwingine anacheza.

“Kuhusu Aucho pamoja na maneno ambayo yanaendelea kwenye mitandao hayatupi hofu, tunahitaji kufanya vizuri na tutaonesha kazi uwanjani,” amesema Bumbuli.

Wachezaji ambao kunahatihati ya Yanga kuwakosa leo Uwanja wa Mkapa ni Khalid Aucho ambaye ni kiungo, Djuma Shaban ambaye ni beki pamoja na Fiston Mayele ambaye ni mshambuliaji.

Previous articleDIWANI SULTAN AMEZINDUA KAMPENI ALAMA ZA USALAMA BARABARANI
Next articleYANGA YAPOTEZA NYUMBANI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here