Na: wandishi wetu, Dar es Salaam.
UONGOZI wa Yanga umesema kikosi kipo vizuri na wachezaji wamejipanga kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United utakaopigwa leo majira ya saa 11 Katika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.
Leo Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa awali dhidi ya Rivers United kutoka Nigeria ambao wa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kauli hiyo aliitoa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa mashabiki wasiwe na presha juu ya wachezaji wao watatu kukosa vibali vya kazi, (ITC).
“Ukizungumzia Yanga hauzungumzii mchezaji mmoja ama wawili ni orodha ya wachezaji wa kazi zaidi ya mmoja na tumesajili wachezaji 30 hii ina maana kwamba akikosekana mmoja mwingine anacheza.
“Kuhusu Aucho pamoja na maneno ambayo yanaendelea kwenye mitandao hayatupi hofu, tunahitaji kufanya vizuri na tutaonesha kazi uwanjani,” amesema Bumbuli.
Wachezaji ambao kunahatihati ya Yanga kuwakosa leo Uwanja wa Mkapa ni Khalid Aucho ambaye ni kiungo, Djuma Shaban ambaye ni beki pamoja na Fiston Mayele ambaye ni mshambuliaji.