Home SPORTS YANGA KUKODI NDEGE KUWAFUATA WAPINZANI WAO

YANGA KUKODI NDEGE KUWAFUATA WAPINZANI WAO

Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.

VIONGOZI ya  Yanga SC wanatarajia kuondoka Ijumaa kwa ndege ya kukodi kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Rivers United.

Katika ndege hiyo ya Shirika la Tanzania, ATCL – Yanga imetoa nafasi pia kwa mashabiki kusafiri kwa gharama ya dola 1200 Economy na 2200 Business.

Kwa taarika Katika mtandao wao Yanga wametoa taarifa kuwa “Yanga wanawaalika wanachama wapenzi na mashabiki kujumuika pamoja katika safari ya kwenda kupindua meza Kibabe huko Nigeria.

Hata hivyo gharama ya safari ni USD 1, 200 kwa daraja Economy na USD 2,200 kwa daraja la Business ikijumuisha pia vipimo vya Covid-19 Dar na Nigeria. Safari ni Ijumaa September 17 na kurudi ni Jumapili Septemba 19, usafiri ni  Airbus A 220-300, Air Tanzania,”.

Yanga wanaenda wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa kipigo Cha 1-0 Jumapili uliochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Ili Yanga wapate ushindi watatakiwa kushinda 2-0 Jumapili kwenye mchezo wa marudiano Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini Port Harcourt, Nigeria.

Lakini pia wakishinda 1-0 mchezo utaamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.

Previous articleMHE.DKT.KIKWETE – NCHI INAKWENDA VIZURI , SAMIA ANALETA MATUMAINI YA LEO NA KESHO
Next articleWAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA DKT. STERGOMENA TAX
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here