Na: Stella kessy, DAR ES SALAAM.
CHAMA cha wushu Tanzania kimeaandaa tamasha la sanaa ya mapigano itakayoyofanyika Oktoba 10 na 11 mwaka huu mkoani Dar es salaam litakalohusosha michezo yote ya mapigano kwa lengo kuinua sanaa hiyo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari leo mratibu wa mkuu wa tamasha hilo,Sempai Kapipi alisema kuwa maandalizi yamekamika na wanalengo la kutengeneza na kuinua na kuwaandaa vijana waliopo mitaani na mashuleni kuwa wapiganaji wazuri wa sanaa hizo za mapigano katika ngazi ya kitaifa.
Alifafanua kuwa katika sanaa ya mapigano ikiwemo chama cha WUSHU Tanzania, chama cha Judo, chama cha Taekwando, TPBRC na chama cha KickboxingTanzania.
Aliongeza kuwa ni mashindano ya kwanza na ya kihistoria katika tasnia hizi za sanaa za mapigano ambayo kwa mara ya kwanza watashiriki vyama vyote katika fani.
Hata hivyo aliwaomba wadau wa watanzania kijitokeza kwa wingi kuja kushuhudia tukio hili muhimu na kihistoria katika fani ya sanaa ya mapigano lakini pia itakuwa ni mwanzo mzuri wa maendeleo wa muendelezo wa matukio matamasha na mashindano hayo yatakayo jumuisha fani zote katika vyama vyote vya sanaa na mapigano.