Home SPORTS SIMBA YASHINDWA KUUNGURUMA MARA

SIMBA YASHINDWA KUUNGURUMA MARA

Na: Mwandishi wetu.

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Simba SC wametoka  sare ya bila kufungana na wenyeji, Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.

Huku kwa upande wa nahodha na mshambuliaji wa kikosi cha simba John Bocco   kukosa mkwaju  wa penalti kupanguliwa na kipa Mganda, Cleo James Ssetuba dakika ya 90.

Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, dodoma jiji waliibuka ushindi  wa bao 1-0 bao pekee la Cleophace Mkandala dakika ya 33 limewapa  dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya, bao la Peter Mapunda dakika ya 90 na ushei limeipa Mbeya City ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

Previous articleWATANO YANGA KUIKOSA KAGERA SUGAR
Next articleWUSHU YAANDAA TAMASHA KUBWA LA SANAAYA MAPIGANO DAR.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here