Home SPORTS WATANO YANGA KUIKOSA KAGERA SUGAR

WATANO YANGA KUIKOSA KAGERA SUGAR


Na: Mwandishi wetu 

NYOTA watano  wa Yanga kesho wataukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar  utakaochezwa katika dimba la Kaitaba  Mkoani Bukoba.

Kauli hiyo ilitolewa jana naMkuu wa Kitengo cha Habari  Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa nyota ambao wataukosa huo mchezo kutokana na sababu mbalimbali.

Miongoni mwa nyota hao ni pamoja na kuhusu wachezaji ambao wamebaki ni Said Ntibanzokiza,’Saido’ ambaye alikosekana pia kwenye mchezo dhidi ya Simba ule wa Ngao ya Jamii.

Yupo beki Yassin Mustapha ambaye amepewa program maalumu kwa ajili ya kurejea kwenye ubora wake baada ya kuwa nje kwa muda akitibu majeraha yake.

 Mukoko Tonombe huyu anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliipata kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho mbele ya Simba, Uwanja wa Lake Tanganyika pia yupo Mapinduzi Balama ambaye naye bado hajawa fiti.

Nyota mwingine ni Dickson Ambundo ambaye aliumia kwenye mazoezi wakati wa maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here