Home BUSINESS WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE 31 KUTOKA MIKOA MBALIMBALI WAFANYA ZIARA MAALUM YA...

WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE 31 KUTOKA MIKOA MBALIMBALI WAFANYA ZIARA MAALUM YA KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA

 

Na:Mwandishi Wetu, IRINGA.

KUNDI la Waandishi wa Habari Wanawake 31 kutoka Mikoa na vyombo mbalimbali wamefanya ziara maalum ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyoko mkoani Iringa kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini ambapo wanataraji kufanya ziara Kama hiyo katika hifadhi mbalimbali zilizopo hapa nchini.

Wakiwa mkoani humo walipata fulsa ya kuzungumza na Kitengo cha mahusiano ya Jamii kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambapo imeeleza kujikita katika kutoa elimu ya uhifadhi kwa waanchi wanaoishi karibu na maeneo ya uhifadhi hiyo.

Hifadhi ya hiyo ya Rauha ina ukubwa wa Squre mita 20,226 ikiwa ni hifadhi ya pili kwa ukubwa nchini ikitanguliwa na hifadhi ya Kwanza ya Nyerere yenye Squre mita 30,893.

Akizungumza na waandishi wa habari hao wanawake wakiwa katika hifadhi hiyo kwa lengo la kuwahamasisha wanachi kutembelea na kuwekeza katika hifadhi mbalimbali , Ofisa uhifadhi kitengo cha mahusiao ya jamii Immaculata Mbawe amesema tayari takribani Sh 3 bilioni zimetumika katika miradi ya maedeleo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo.

Immaculata amesema Hifadhi hiyo ya Ruaha imepakana na Wilaya tano za Mufindi, Iringa, Chunya, Mbarari na Wilaya ya Chamwino ambazo ziko katika mikoa mitatu ya Dodom,Iringa na Mbeya ikiwa zaidi ya vijiji 135 vinavyotakiwa kufikiwa na elimu ya uhifadhi pamoja.

Kitengo hicho kimekuwa kikihusika katika utoaji wa miradi ya kimaendeleo kwenye jamii zinazozunguka hifadhi ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya uhifadhi wa maliasili, ujenzi wa madarasa,zahanati madawati, maktaba na Vifaa vinavyosaidia katika maendeleo ya jamii.

Amesema wamewekeza katika vikundi vitatu vya ufugaji wa Nyuki ili wananchi waweze kuondokana na dhana ya uharibifu Mazingira katika maeneo ya Hifadhi hiyo ikiwa lengo kuu ni kutunza hifadhi zetu.

Naye Ofisa Uhifadhi kitengo cha Utalii Ahmedy Nassoro amesema kwa takwimu za kuanzia mwezi Juni mpaka Agost mwaka huu kumekuwa na ongezeko la wageni mpaka 1000 kwa mwezi tofauti na kipindi cha awamu ya kwanza na pili ya Ugonjwa wa Covid ulipoanza kwani hapakuwa kabisa na wageni hifadhini hapo.

“Hifadhi hii ina upekee tofauti na hifadhi zingine ikiwa ni pamoja na makundi makubwa ya Tembo , Nyati na Tandala ambao wako kwa wingi kulingana na eneo na maumbile kuwa na nyika nzuri na rafiki kwa wanyama,”amesema

Amefafanua kuwa watalii wa ndani na nje ya nchi huwa kuna mzunguko wa safari za gari usiku na mchana ambapo mgeni ataweza kuona wanyama wote wanaozunguka hifadhini hapo, hoteli mbalimbali z kulala na hiuduma zote za kijamii.

Kwa upande wake mhifadhi kitengo cha Ikolojia Halima Kiwango akieleza waandishi hao wa habari wanawake hifadhi historia ya hiyo amesema kumekuwa na upekee kwa hifadhi kuwa na muingiliano wa aina kuu mbili za uoto wa Migunga uliopo kaskazini mwa hifadhi na Miombo uliopo kusini kwa kukutana pamoja na kusababisha kuwepo na muingiliano wa wanyama katika katika eneo lote la hifadhi.

Pia katika hifadhi hiyo kumekuwa na changamoto ya kukauka kwa mto ruaha ambao ndio tegemeo la wanyama kupata maji na mpaka sasa kumekuwa na juhudi mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa kwa serikali ,wataalamu na jamii inayozunguka kuweza kutunza vyanzo vya maji.

‘’Kama tunavyojua maji ni uhai hivyo nitoe wito kwa wananchi kulinda vyanzo vya maji hasa katika maeneo ya uhifadhi na sehemu nyingine kwa kuwa maji ni tegemeo la sekta nyingi hivyo tuhahakikisha tunayatumia na kuyalinda,”amesema Amina.

Awali Askari Muhifadhi daraja la pili Munga Mtaiko alisema kuwa katika ziara hii ya waandishi wa Habari wanawake tumefanikiwa kuwaona wanyama wakiwa katika makundi ikiwa ni Tembo ambao hutembea umbali mrefu kutafuta maji na malisho, Swala ambao huwa zaidi ya 60 ikiwa ni majikee wote na mwanaume mmoja katika kundi zima.

Akiongea baada ya kumaliza ziara hiyo ya siku mbili hifadhini hapo Mratibu wa kampeni hiyo ya kuhamasisha Utalii na uwekezaji kupitia waandishi wa habari wanawake Nchini, Maria Mwakibete amesema kuwa kwa kuanza na hifadhi ya Taifa ya Ruaha ni katika kuhamasisha utalii na fursa za uwekezaji zinazopatikana katika mikoa mbalimbali ili kuondoa dhana ya utalii kufanywa na wageni kutoka nchi na mataifa mbalimbali na sio wazawa.

Kwa upande wao waandishi wa habari wakiwemo wameeleza kufurahishwa na ziara hiyo ambayo wanaamini itakuwa na tija kubwa kwa taifa kwani kwa kuitangaza kwa umoja wao ni rahisi watu ambao walikuwa hawaijui hifadhi hiyo na sifa zake Sasa watazijua.

“Tumefurahishwa sana na huduma mbalimbali za kijamii zinazotolewa hifadhini hapo ikiwa ni pamoja na mazingira mazuri yaliyo rafiki kwa ajili ya malazi , chakula pamoja na burudani zinazopatikana hifadhini hapo.

“Zaidi tumefurahishwa baada ya kusikia historia ya Wanyama aina ya Tandala wanaokuwa kwenye kundi la zaidi ya 60 ikiwa ni wanawake na kati yao mmoja pekee ndio dume ambaye anamiliki kundi hilo kubwa na pia kuwazalisha yeye pekee baada yakushinda mapigano dhidi ya tandala wengine wakiume,”amsema.

Previous articleMAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MKUTANO WA AFRICA – CARRICOM
Next articleMAGAZETI YA LEO J.TANO SEPTEMBA 8,2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here