Home LOCAL MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MKUTANO WA AFRICA – CARRICOM

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MKUTANO WA AFRICA – CARRICOM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na washiriki mbalimbali ambao ni wakuu wa Nchi na Serikali wakati aposhiriki mkutano wa kwanza wa Afrika na Umoja wa Nchi za “Carribbean”(Africa – CARRICOM Summit) uliofanyika kwa njia ya mtandao. Septemba 7, 2021.

PICHA – OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Septemba 7, 2021 amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa wa kwanza wa  Afrika na Umoja wa Nchi za “Carribbean”(Africa – CARRICOM Summit) uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Akizungumza katika mkutano huo, Makamu wa Rais amesema nchi za afrika na za “ Carribean” zinafanana katika katika masuala mbalimbali hasa katika nia ya kuhitaji maendeleo ya haraka hivyo kuwepo na ushirikiano baina nchi hizo kutaongeza kasi ya maendeleo pamoja na kuwa na sauti ya pamoja kwa manufaa ya mataifa yote ndani ya umoja huo.

Makamu wa Rais amesema Tanzania inaunga mkono mapendekezo ya kuwepo kwa siku maalum ya umoja huo pamoja kuziasa nchi washiriki wa mkutano huo kuendelea kutoa msukumo wa kupatikana kwa chanjo kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona katika nchi zinazoendelea zenye uhitaji mkubwa wa chanjo hiyo.

Mkutano huo umejadili ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo Uchumi wa Bluu, Afya, Teknolojia  Mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kudhibiti ugojwa wa Corona.

Mkutano huo umehudhuriwa na wakuu wa nchi na serikali kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na Carribean.

 

Previous articlePRF. KITILA ATEUA WAJUMBE WA BODI YA CAMARTEC,
Next articleWAANDISHI WA HABARI WANAWAKE 31 KUTOKA MIKOA MBALIMBALI WAFANYA ZIARA MAALUM YA KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here