Mfanyabiashara maarufu wa Mavazi anaetengeneza na kusambaza jezi za timu ya Simba Fredy Vunjabei akizungumza kwenye mkutano namna alivyojipanga kimauzo na kuwafikia mashabiki mbalimbali wa timu hiyo popote nchini na nje ya nchi. PICHA NA: HUGHES DUGILO)
Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo Septemba 1 imetangazatarehe rasmi ambayo jezi zao mpya zitazinduliwa kwaajili ya msimu wa ligi kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Ezekiel Kamwaga ni Kaimu Msemaji wa Klabu ya Simba anafafanua kuwa Klabu hiyo ya Msimbazi ya Jijini Dar es Salaam iliingia makubaliano na Fredy Vunjabei ya kuuza na kusambaza jezi za Simba kwa mkataba wa Sh. Bilion mbili na kwamba katika siku hiyo ya Septemba 4 kutafanyika uzinduzi rasmi.
“Kabla ya Klabu ya Simba kuingia mkataba na Vunja Bei tulikuwa na Umbro na tulikuwa na mafanikio makubwa na Simba ni sehemu ya mafanikio.Tunafahamu biashara ya jezi na vifaa vya michezo ndio biashara kubwa duniani ,zaidi ya trilioni 84 zinapatikana katika biashara ya vifaa vya michezo na jezi,”amesema Kamwaga.
kwa upande wake mfanyabiashara Fred Vunja Bei amesema kuwa wao kama wasambazaji wa jezi hizo watahakikisha wanaoyesha uaminifu mkubwa kwenye zoezi zima nakwamba kila mwanasimba ataweza kupata jezi hiyo popote pale alipo ndani na nje ya nchi.
“Simba imetuamini na sisi tutaonesha uaminifu, hakuna jezi ambayo imetengezwa ikavuja hadi sasa.Kwenye mitandao zimewekwa jezi nyinyi lakini ukweli jezi yetu haijavuja mpaka sasa.Jezi zetu za msimu huu zitazinduliwa Septemba 4 mwaka huu.
“Tutakuwa na wadau wa michezo kutoka sehemu mbalinbali, tumejipanga, tunajua ukubwa wa Simba, hivyo uzinduzi wetu tutaufanya kwa ukubwa wa Simba, kutakuwa na uzinduzi wa aina mbili, Septemba 4 watazindua kuanzia saa 11 hadi saa tatu usiku,na itakuwa live Azam TV, na uzinduzi wa aina ya pili utakuwa wa mtandaoni kwa ajili ya kuuza jezi mtandaoni,”amesema Fred Vunja Bei.
Mwisho.