Home ENTERTAINMENTS MSANII WA BONGO FLEVA WHOZU AZINDUA WIMBO MAALUM WA SIMBA SC

MSANII WA BONGO FLEVA WHOZU AZINDUA WIMBO MAALUM WA SIMBA SC

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Whozu akizungumzia wimbo wake mpya maalum kwaajili ya timu ya Simba kuelekea kwenye Sherehe za Simba Day Septemba 19,2021. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)

 DAR ES SALAAM 

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Whozu ametunga wimbo maalum kwa ajili ya wanachama,mashabiki na wapenzi wa Klabu ya Simba ambao unakwenda kwa jina la Simba ni Noma.

Akizungumza leo Septemba 1,2021 Wohzu amesema ameamua kutunga wimbo huo kutokana na mapenzi yake makubwa na klabu ya Simba,yeye ni Simba kindakindaki,hivyo ameamua kutunga wimbo huo.

“Tunafahamiana wengi,mimi ni msanii wa muziki wa kizazi kipya,nimekuwa nikitumia talanta yangu katika sanaa ya muziki, hivyo nimeamua kitengeneza wimbo maaalum kwa ajili ya Simba,mashabiki wa Simba ,nimefanya hivyo kwasababu ya wachezaji wa Simba.

“Simba ni bingwa hata wasemeje, nimetumia ubunifu kidogo,sijaimba kwa Singeli bali nimechanganya ladha, nimetumia Singeli kidogo, bongo fleva kidogo na bolingo kidogo, nimechanganya ili kupata kitu kizuri, siko mwenyewe nimemshirikisha Donat Mwanza anayetokea Congo.

“Mwanamuziki huyo ameshawahi kuhiti na Bana Congo, ana wimbo wake ambao umekuwa maarufu sana. Lakini katika mazungumzo yangu na Donat Mwanza ni shabiki mkubwa wa Simba, hivyo haikuwa ngumu kumshawishi, kumshirikisha wimbo huo na tumeufanya kwa Kiswahili,Wimbo unaitwa Simba ni Noma.

“Simba ni  Noma, wimbo umerekodiwa na upo tayari wimbo ni mzuri sana na umeshatoka, wimbo huo ni maalum kwa ajili ya Simba, ni wimbo wa kushabikia Klabu, kokote uliko mwana Simba tembea kifua mbele,jidai wewe ni mshindi, kikubwa naipenda Simba ,ni Simba kindaki ndaki, tutauwimbo na mashabiki zetu, tutauumba kiubibgwa,amesema Wohzu.

Mwisho

Previous articleSIMBA SC YATANGAZA TAREHE YA KUZINDUA JEZI ZAO MPYA.
Next articleRC DAR APIGA MARUFUKU MICHANGO SHULENI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here