Home SPORTS SIMBA QUEEN Vs LADY DOVES PATACHIMBIKA LEO.

SIMBA QUEEN Vs LADY DOVES PATACHIMBIKA LEO.

 Na: Mwandishi wetu, NAIROBI.

KIKOSI cha Simba Queen leo kitashuka dimbani kuchuana na  Lady Doves katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu  katika Michuano ya  Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ya Wanawake, CECAFA Samia Cup leo Uwanja wa Moi Kasarani Jijini Nairobi, Kenya.

Mchezo huko utapigwa majira ya mchana huku benchi la ufundi limepanga kupanga kikosi chenye ushindani ili kinyakua nafasi hiyo ya tatu katika michuano hiyo.

Hata hivyo katika mchezo huwa wa leo kikosi cha  Simba  kitamkosa  nahodha wao Violeth  Nicholaus ambaye ni majeruhi ambaye aliumia katika mchezo dhidi ya Vihiga Queen.

Mchezo huo dhidi ya Lady  Doves utazikutanisha timu hizo kwa mara ya pili baada ya ule wa hatua ya makundi  ambao Simba ililazimika kutoka sare ya bila kufungana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here