Home SPORTS SIMBA KUJIPIMA NGUVU NA TP MAZEMBE KESHO

SIMBA KUJIPIMA NGUVU NA TP MAZEMBE KESHO

 

Na: Stella kessy, DAR ES SALAAM.

MABINGWA wa ligi kuu Tanzania Bara  kesho wanashuka  dimbani dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo, ikiwa mechi ya kirafiki ya kimataifa ikiwa ni maandalizi ya mwisho kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza leo na vyombo vya Habari Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomez,Amesema kuwa kikosi kipo vizuri kwa ajili ya mechi dhidi ya Tp Mazembe pamoja na msimu mzima wa ligi kuu na michuano ya kimataifa.

“Ninajua ni mechi kubwa tunayokutana nayo Lakni naweza kusema kuwa kikosi kimefanya maandalizi vyema kwaajili ya msimu huu mpya unaotarajiwa kuanza Kwa msimu mpya wa ligi”anasema.

 Kwa upande wa nahodha  wa timu John Bocco alisema kuwa kikosi kimejipanga vyema  kufanya vizuri kwa mchezo wa kirafiki. “Mimi ninaomba mashabiki wajitokeze Kwa wingi  kesho kikosi kipo vizuri malengo yetu kama timu tumefanya vizuri na kuonyesha mashabiki jinsi gani tumejipanga na  hii itakuwa ni mechi  ya kimaifa ya awali ambayo mashabiki zetu watashuhudia hivyo naomba wajitokeze”alisema.

Aliongeza kuwa wachezaji wote wapo vizuri kwa ajili ya kupambana katika michuano ya ligi na kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here