Home SPORTS TP MAZEMBE WATUA DAR

TP MAZEMBE WATUA DAR


Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM. 

MABINGWA Afrika, TP Mazembe wamewasili  leo Tanzania kwa ajili ya  mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa kesho, Septemba 19, Uwanja wa Mkapa.

Mbali na kutwaa taji hilo kubwa Afrika mwaka 1967,1968,2009,2010 na 2015 pia timu hiyo ilitwaa mataji mawili ya Kombe la Shirikisho ilikuwa ni 2016 na 2017 itapimana ubavu na Simba.

Akizungumza   Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kuwa kikosi Cha TP Mazembe kimewasili salama.

“Taratibu zote zipo tayari kuanzia masuala ya tiketi mpaka mapokezi hivyo wale ambao wanamashaka juu ya ujio wa TP Mazembe tayari na mpira utachezwa kama kawaida,” amesema Kamwaga.

Pia Simba walitoa taarifa kuhusu kushughulia usumbufu wa upatikanaji wa tiketi ambao umekuwa ukijitokeza kwa mashabiki wao katika harakati za kukata tiketi hizo.

Previous articleNAIBU WAZIRI WA VIWANDA EXAUD KIGAHE ATOA NENO KWA WATUMISHI WA WMA
Next articleSIMBA KUJIPIMA NGUVU NA TP MAZEMBE KESHO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here