Home BUSINESS RC: SENYAMULE: MAANDALIZI MAONESHO YA NNE YA SEKTA YA MADINI YAMEKAMILIKA

RC: SENYAMULE: MAANDALIZI MAONESHO YA NNE YA SEKTA YA MADINI YAMEKAMILIKA

Na: Tunu Bashemela, GEITA.

Maandalizi katika kuelekea Maonesho ya nne ya Teknolojia ya Uwekezaji katika Sekta ya Madini Mwaka huu yanayofanyika Mkoani Geita yamekamilika huku kukiwa na mwitikio mkubwa wa Wajasiriamali, Makampuni na Mashirika mbalimbali kushiriki.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mh. Rosemary Senyamule jana septemba 14 alitembelea mabanda mbalimbali ya washiriki katika maonesho hayo katika uwanja wa Bombambili EPZ na kujionea namna ambavyo washiriki hao wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho tayari kwaajili ya kushiriki maonesho hayo yanayotarajiwa kuanza rasmi septemba 16 mwaka huu.

Maandalizi yapo vizuri kila kitu kipo sawa hapa na washiriki mbalimbali wameshafika na kuandaa mabanda yao tayari wakiwemo wajasiriamaliā€¯alisema RC Senyamule.

Katika zoezi hilo Mhe. Senyamule aliongozana na wajumbe wa Kamati ya maandalizi wa manesho hayo huku Mwenyekiti wa kamati hiyo akionekana kufurahishwa na mwitikio mkubwa wa washiriki kwenye maonesho hayo.

Aidha katika kupita katika mabanda hayo Mh Mkuu wa Mkoa alipata nafasi ya kuzungumza na wajasiriamali wa vinywaji na chakula ambao tayari wameshaandaa mabanda yao tayari kwa kutoa huduma katika maonesho hayo huku wakimuhakikishia Mkuu huyo wa Mkoa kuwa wamejiandaa vema kutoa huduma  nzuri kwa wateja na wananchi wote kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here