Home LOCAL RC MAKALLA ATOA ONYO BIASHARA YA NGONO UWANJA WA FISI.

RC MAKALLA ATOA ONYO BIASHARA YA NGONO UWANJA WA FISI.– Atoa Wiki moja kukomeshwa kwa Biashara hiyo.

– Aelekeza Jeshi la Polisi kutuma Askari waliovaa kiraia na kujifanya wateja.

– Wananchi walalamikia Watoto wadogo kufanyishwa biashara ya ngono.

Na: James Lyatuu, DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa Wiki moja kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanadhibiti watu wote wanaofanya biashara ya Ngono kwenye eneo la Manzese Uwanja wa Fisi baada ya suala hilo kulalamikiwa na Wananchi.

Malalamiko hayo yametolewa wakati wa Mwendelezo wa ziara ya kusikiliza na kutatua Migogoro ya Wananchi Jimbo la Kinondoni ambapo wamedai kuwa imefikia hatua biashara hiyo inahusha pia utumikishaji wa kingono kwa watoto wadogo Jambo ambalo ni kinyume na sheria na maadili.

Kutokana na hilo RC Makalla amewaelekeza Jeshi la Polisi kuwatuma askari watakaovaa nguo za Kiraia na kuwanasa watu wote wanaofanya biashara ya ngono.

Aidha RC Makalla ameelekeza Viongozi wa kata na Mtaa huo kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kumaliza suala hilo.

Previous articleMNADHIMU MKUU JWTZ AMWAGIA SIFA KAPTENI SEMUNYU NA ASKARI WACHEZAJI TAARIFA KUZIFIKISHA KWA MKUU WA MAJESHI
Next articleBRELA YAFANYA USAJILI NA KUTOA VYETI PAPO KWA HAPO KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here