Home LOCAL RC MAKALLA APIGA MARUFUKU UJENGAJI HOLELA WA VIBANDA VYA BIASHARA MASHULENI.

RC MAKALLA APIGA MARUFUKU UJENGAJI HOLELA WA VIBANDA VYA BIASHARA MASHULENI.

 
Na: James Lyatuu, DAR ES SALAAM.
– Asema vinahatarisha usalama wa wanafunzi na kuweka mazingira ya Wanafunzi kudanganywa.

– Wazazi wahofia usalama wa Afya za watoto wao.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amepiga marufuku ujengaji holela wa Vibanda vya biashara Mashuleni Kutokana na utaratibu huo kuhatarisha usalama wa wanafunzi baadhi ya watu kutumia mwanya huo kuwarubuni watoto wa shule.

Kutokana na hilo RC Makalla ameamuru Wakuu wa shule kusimamia kuondolewa kwa Vibanda vyote vilivyojengwa kwenye maeneo ya shule.

Aidha RC Makalla amesema ni vyema Wanafunzi wakapata mahitaji yao kwenye duka la shule au ukafanyika mchujo watu wachache maalumu wa kutoa huduma ambao wanatambulika na uongozi wa shule ili ata ikitokea tatizo iwe rahisi kujua chanzo Cha tatizo.

Hayo yote yamejiri wakati wa Mwendelezo wa ziara ya RC Makalla ya utatuzi wa Migogoro ya Wananchi Jimbo kwa Jimbo ambapo leo ilikuwa zamu ya Wananchi wa Jimbo la Segerea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here