Home LOCAL RC MAKALA AWATAKA WANANCHI WAJIEPUSHE NA MATAPELI MAGOMENI KOTA

RC MAKALA AWATAKA WANANCHI WAJIEPUSHE NA MATAPELI MAGOMENI KOTA

NA: HERI SHAABAN

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam amewataka wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam , kujiepusha na matapeli katika mradi wa nyumba za Magomeni Kota Wilaya ya Kinondoni wanaowaomba pesa kwa ajili ya kupanga katika nyumba hizo za mradi wa Makazi waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota.

Mkuu wa Mkoa Makala aliyasema hayo Dar es Salaam Leo ,katika ziara yake kuangalia maendeleo ya mradi huo ambapo kwa sasa umefikia asilimia 95.

“Maendeleo ya mradi wa nyumba za Magomeni Kota umefikia hatua za mwisho nyumba hizi wataka wakazi wa eneo hilo Kaya 644 wanatambulika sio wananchi wengine ” alisema Makala.


Makala alisema nyumba za Magomeni Kota zinajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)   mradi ulianza kutekezwa October 2016 ikiwa ni ahadi wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania Hayati  Dkt.John Pombe Magufuli , ambapo kwa sasa tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassani Suluhu  kwa usimamizi mzuri mpaka mradi umefikia hatua za mwisho

Makala amewatoa hofu kaya za Wakazi wa Magomeni kota wasiwe na wasiwasi mradi ukikamilika watakaa katika nyumba hizo hivyo matapeli wasipotoshe umma .

Aliagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama kuwatafuta kundi hilo la matapeli linalopotosha umma kwa madai kuwa wao ndio wanasimamia kupangisha nyumba hizo wakati si kweli eneo hilo halina nyumba za kupanga.

Alisema mradi huo gholofa tano gharama ya mradi shilingi bilioni 52 nyumba 656  wakazi 3000 eneo lingine la Machinga na vyoo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Tanzania TBA Said Mndeme ,alisema kwa sasa mradi huo umefikia asilimia 99 kwa sasa wanafunga Trasfoma  tano Mara baada hapo kazi itakuwa imeisha .

Mkurugenzi wa TBA Mndeme alisema mradi huo ukikamilika wakazi wa eneo hilo watawakiki majina upya baada hapo watawapa Elimu katika kuishi katika Majengo hayo.

Alisema majengo hayo ni ya kisasa hivyo amewataka wakazi wa Magomeni kota Wilaya Kinondoni kuyatunza vizuri  watakaa katika majengo hayo bure kwa miaka mitano.
Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here