Baadhi ya mawakili waserikali ambao wapo zaidi ya 100 wakifuatilia jambo katika mkutano wao wa baraza la wafanyakazi Ofisi ya wakili mkuu wa serikali mkutano uliofanyika mkoani Arusha.
|
NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Ofisi ya wakili mkuu wa serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021 imeweza kuokoa zaidi ya billion 541 katika mashauri ya madai na usuluishi, fedha ambazo zingeweza kulipwa kwa wadai kama wasingeiwakilisha serikali vizuri kwenye mashauri ya madai na usuluishi mbalimbali waliyoyafanya.
Hayo yamesemwa na kaimu mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi la ofisi ya ya wakili mkuu wa serikali Dkt Boniphace Luhende katika kikao Cha kwanza cha baraza hilo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo alisema kuwa kwa upande wa mashauri ya madai kiasi kilichookolewa ni shilingi 540,398,775,272 huku upande wa mashauri ya usuluishi kiasi kilichookolewa ni shilingi 685,474,629 na Dola za kimarekeni 1,152,572,523.
“Baadhi ya mashauri ya madai na usuluishi tunayoishughulikia hutokana na kukiukwa kwa masharti ya mikataba mbalimbali inayoingiwa na serikali au tasisi zake, umiliki wa ardhi, kodi, madai ya kikatiba na haki za binadamu ambapo utumia njia ya usuluishi kwa njia ya majadiliano na kufungau kesi mahakamani,” Alieleza Dkt Luhende.
Dkt Luhende alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa ofisi hiyo February 12,2018 imekuwa ikitekeleza majukumu yake ya uratibu, usimamizi, ushauri na uendeshaji wa mashauri yote ya madai na usuluishi yanayofunguliwa dhidi ya serikali na taasisi zake ndani na nje ya nchi.
“Napenda kuwahakikishia kuwa titaendelea kufanya kazi kwa weledi na uadilifu mkubwa na kutekelezwa ipasavyo malengo ya kuanzishwa kwa ofisi hii na tunatambua matarajio ya serikali na taasisi zake kwetu hivyo tunaahidi kuwa tutajitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuhakikisha tunatekeleza majukumu hayo na kufikia matarajio ya serikali,” Alisema Dkt Luhende.
Aidha alisema kuwa matunda ya kuwa na baraza la wafanyakazi mahala pa kazi yameanza kuonekana ndani ya ofisi ya wakili mkuu ambayo ni pamoja na kushirikisha katika uandaaji wa nyaraka mbalimbali kama vile bajeti ya kila mwaka na mpango kazi wa kila mwaka pamoja na mkakati wa OWMS wa miaka mitano(2021/2026).
Alifafanua kuwa ili kufikia malengo yanayotokana na vipaumbele vya nchi ambavyo vimewezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati, kuvutia wawekezaji na ujenzi wa viwanda Kama serikali hawana budi kufanya kazi kwa ushirikiano ili changamoto zinazokwamisha maendeleo ziweze kutatuliwa kwa haraka.
“Katika kutekeleza majukumu yetu tunazingatia Katiba, Sheria, Kanuni, Taratibu, Miongozo mbalimbali pamoja na Mila na Desturi zinazosimamia shughuli za serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania,”Alisema.
Sambamba na hayo pia alisema kuwa katika kutekeleza majukumu yao kwa mwaka 2020/2021 walikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutokuwq na muundo wa utumishi katika ofisi hiyo, upungufu wa watumishi wenye ustadi maalum, ukosefu wa umiliki wa jengo, upungufu wa magari, huduma mtandao kwenye masijala ya Sheria pamoja na maktaba Mtandao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa TUGHE tawi la ofisi ya wakili mkuu wa serikali Mtani Songorwa alisema kuwa kazi wanazozifanya ni kazi zinazohusiana na jamii pamoja na watanzania wote kwani kesi inapofunguliwa dhidi ya serikali, serikali inahusu wananchi wote hivyo zinapoenda vizuri na serikali kushinda matarajio ya wananchi yanafikiwa kupitia uendeshaji wa kesi.