Anaripoti: Richard Mwaikenda, CCM Blog, Ludewa.
MBUNGE wa Ludewa, Joseph Kamonga ametoa ng’ombe kwa ajili kitoweo kwa wanaoshiriki Tamasha la mashindano ya ngoma ya asili ya Mganda jimboni humo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi Kamonga ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mashindano hayo ya siku 3 ameipongeza kamati ya maandalizi kwa kufanikisha tamasha linaloshirikisha maboma 15 kutoka wilaya za Mbinga, Nyasa na Ludewa yenyewe.
Amesema kuwa mashindano hayo ya ngoma ya asili yaliyofanyika katika Kitongoji cha Nkinila, Kijiji cha Lifua Kata za ya Luilo ni muhimu sana kwani husaidia kujenga mahusiano, huleta burudani lakini pia amani na upendo na kwamba imo hata kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. (PICHA NA: RICHARD MWAIKENDA).
“Kwa hiyo ndugu zangu Michezo , Sanaa na Utamaduni inasisitizwa sana kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Serikali yetu ina wizara mahususi ambayo husimamia mambo ya utamaduni, nimesikiliza nyimbo nimeona wanaimba nyimbo ya kudumisha amani upendo na mshikamano, ambao ulianzishwa wasisi wetu tokea miaka mingi, lakini michezo licha ya kuleta burudani, vile vile inatuburudisha na kujenga mauhusiano mema baina ya jamii,”amesema Kamonga. (PICHA ZOTE NA: RICHARD MWAIKENDA).
Vikundi (maboma) vilivzoshiriki katika mashindano hayo ni:Wilaya za Ludewa;Lihagule,Luilo,Mseto,Idusi,Kiyoho, Nindi, Nsungu na Mzalendo. Nyasa ni;Lituhi,Taifa,Upendo, Uweyo na Shujaa na kutoka Mbinga ni Ndongosi na Lizombo. (PICHA ZOTE NA: RICHARD MWAIKENDA).
Mdau ili nisikuondolee uhondo nakuomba uendelee kuona/kusikiliza kupotia clip hii za video Mwenzekiti wa Kijiji cha Lifua,Msafiri Haule, Diwani wa Kata za Luilo, Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Kamonga na wananchi wakizungumzia tamasha hilo lakini na kuona pia tamasha hilo. Credit – Blog ya Taifa ya CCM