Home SPORTS MABONDIA 20 KUZICHAPA OCTOBA 30,2021 DAR

MABONDIA 20 KUZICHAPA OCTOBA 30,2021 DAR

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

MABONDIA 20 wanatarajia  kuzichapa katika pambano la Mwana Ukome Derby ya Dar es Salaam Oktoba 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kinesi, hapo Jana walitambulishwa  kwenye viwanja vya Las Vegas, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa utambulisho huo, Promota wa mapambano hayo, Mtendaji Mkuu wa PeakTime Media, Kapteni Selemani Semunyu, amesema kutokana na kukubali matakwa ya mashabiki wake ngumi, ameamua kuhamishia michezo hiyo Uwanja wa Kinesi badala ya Beach Kidimbwi.


Amesema anafahamu mashabiki wengi wa ngumi wanatokea maeneo ya Mabibo, Manzese, Mburahati na sehemu nyingine za karibu.

Mapambano makali katika derby hiyo, ni kati ya Ramadhani Shauri na Iddi Pialari, Francis Miyeyusho dhidi ya Adam Kipenga,hayo yatapi

Mabondia wengine watakaopanda ulingoni siku hiyo ni kutoka Jeshi la Wananchi (JWTZ), Selemani Kidunda, Ismail Galiatano,George Bonabucha na Grace Mwakamele.



Wengine ni Hassan Ndonga, Boni Sela Saleh Mkalekwa, James Kibazange na Ally Ngwando

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here